pichani ni Afisa maendeleo ya Jamii kutoka TAMISEMI Hilda mgomapayo,Idara ya Maendeleo ya jamii ya Halmashauri ya Mji wa Makambako ,na Afisa Mipango wa Mkoa wa Njombe wakizungumza na wanakukundi cha Umoja kilichopo mjini Makambako ambapo kikundi cha umoja ni moja ya kikundi nufaika na Mkopo wa serikali kupitia Halmashauri ambapo wamekiri dhahiri kuwa kupitia mkopo huo wameweza kufanya mambo mengi na mazuri hasa kwa kuanzisha mradi wao wa kushona sale za wanafunzi na kuziuza sehemu mbalimbali hususani katika minada ambapo wamepata faida kubwa hali iliyopelekea wanakikundi wote kununua viwanja na kujenga nyumba zao za kuishi pamoja na familia zao .Vijana hao hawakusita kuishukuru serikali ya awamu ya tano chini ya Rais DK John Pombe Magufuli kwa msistizio mkubwa hasa kwa vijana kufanya kazi kwa bidii na kuepuka kukaa bila kazi yoyotea zaidi kuishi kauli ya mheshimiwa Rais ya HAPA KAZI TU mbali na hayo wameishukuru Halmashauri ya Mji wa Makambako kupitia idara ya Maendeleo ya jamii kwa kuwasidia kutoa elimu nzuri ya ujasiliamali kupitia mikutano na vyombo vya habari hususani Radio wakati wa kutoa elimu kabla na mara baada ya kupewa mkopo .
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa