Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako anawatangazia wananchi wote kuwa, Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji wa Makambako litafanyika tarehe 13/11/2019 siku ya Jumatano katika Ukumbi wa mikutano wa LUTHERAN CENTRE jirani na TAZARA saa 3:00 ASUBUHI.
Mkutano huo hufanyika kwa lengo la kujadili Taarifa za maendeleo kila robo ya mwaka wa Fedha, hivyo Baraza litakutana tarehe tajwa kujadili taarifa za robo ya kwanza(Julai, Agosti na Septemba) ya mwaka wa Fedha wa serikali, 2019/2020.
WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa