Na. Lina Sanga
Kauli hiyo imetolewa na Wanafunzi wa Mkoa wa Njombe katika kikao cha uzinduzi wa vitabu vitatu vya muongozo wa elimu Mkoa wa Njombe, kilichofanyika leo shule ya Sekondari Mpechi.
Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wengine, Augenia Mwenda mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya sekondari Mbeyela,amesema kuwa baadhi ya wanafunzi waliofanya makosa mbalimbali hupewa adhabu ya kusimamishwa shule na kuruhusiwa kufika shuleni kufanya mitihani ya kuhitimu masomo, hali inayochangia ongezeko la ziro kwenye matokeo ya mitihani.
Ametoa rai kwa Serikali na Mamlaka za elimu kubadilisha adhabu hiyo ya kumrudisha mwanafunzi nyumbani,bila kujihakikishia kama mwanafunzi huyo atasoma akiwa nyumbani zitolewe, adhabu mbadala kama kuchimba mashimo au kulima na mwanafunzi aendelee na masomo yake ili kuwasaidia wanafunzi kufaulu masomo yao vizuri.
Aidha,wanafunzi hao wamebainisha changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika mazingira ya shule ,kama ukosefu wa uzio kuzunguka mabweni ya watoto wa kike,ukosefu wa maji ya kutosha na uchakavu wa ofisi za walimu.
Pia,wamempongeza Mkuu wa Mkoa wa Njombe kwa kuahidi zawadi kwa walimu,wanafunzi na shule itayofaulisha vizuri ambapo zawadi hizo ni kuanzia laki Tano hadi milioni tano.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa