Na. Lina Sanga
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji Makambako,Mhe. Hanana Mfikwa ametoa shukurani kwa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za Utekelezaji wa Miradi mbalimbali katika Halamshauri ya Mji Makambako ikiwa ni pamoja na miradi ya elimu,Afya,Maji na Barabara.
Mhe. Hanana ametoa shukurani hizo leo,katika mkutano wa baraza la madiwani kwa kipindi cha kuishia robo ya pili (oktoba-desemba) 2021/2022, uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji makambako,hivyo niwajibu wa kila diwani pamoja na timu ya wataalamu kuhakikisha fedha zinazoletwa kutumika vizuri na kukamilisha miradi kwa muda uliopangwa.
Mhe. Hanana amesema kuwa licha ya fedha za ujenzi wa Madarasa na Zahanati bado Serikali inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Miradi mbalimbali,ambapo Halmashauri ya Mji Makambako imepokea milioni 470 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari kitisi na milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati ya kitandililo.
“Halmashauri yetu tulipokea fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa na bweni moja la watoto wenye ulemavu kwa fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko 19,lakini bado fedha zingine zinaletwa kwa ajili ya miradi mbalimbali,ni wajibu wetu kumshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa fedha hizo na tunamuhakikishia kutumia vizuri fedha hizo, kusimamia miradi vizuri na kuhakikisha inakamilika kwa wakati”, alisema Mhe. Hanana.
Halmashauri ya Mji Makambako ilipokea jumla ya shilingi Bil. 1.2 ambapo milioni 840 zimetumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa na bweni moja la watoto wenye ulemavu kwa fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko 19 na milioni 300 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya dharura ya huduma ya afya,
Aidha Mamlaka ya Maji Mji Makambako (MAKUWASA) imepokea jumla ya shilingi mil. 137 kwa ajili ya miradi ya maji na miradi hiyo imeanza kutekelezwa,pia kiasi cha shilingi mil. 437 zimetengewa bajeti kupitia fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko 19 kwa ajili ya Miradi ya Maji.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa