Na. Lina Sanga
Ikiwa imebaki siku moja kuhitimisha zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura, baadhi ya wananchi ambao hawakua na vitambulisho vya mpiga kura,waliopoteza vitambulisho au vitambulisho vyao kuharibika na ambao watatimiza miaka 18 tarehe ya uchaguzi mkuu 2025 na waliohama Kata, wamefanikiwa kuboresha taarifa zao na kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura na kuwa wapiga kura katika maeneo wanayoishi, kwa ajili ya kumchagua diwani, Mbunge na Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na uandikishaji wa wapiga kura wapya katika Halmashauri ya Mji Makambako na Mkoa wa Njombe kwa ujumla,lilianza rasmi januari 12,2025 na litahitimishwa kesho januari 18,2025 saa 12:00 jioni.
Wananchi ambao wana sifa za kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi Mkuu 2025, na bado hawajajiandikisha au kuboresha taarifa zao wanatakiwa kufanya hivyo kesho kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni ,kwenye vituo vyote vya uandikishaji katika Kata zote 12 za Halmashauri ya Mji Makambako.
Kauli mbiu ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura inasema " Kujiandikisha kuwa mpiga kura, ni Msingi wa Uchaguzi Bora".
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa