Na.Lina Sanga
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Makambako leo,limeidhinisha rasimu ya mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 yenye jumla ya bil. 28.75 ambayo Halmashauri ya Mji Makambako inakusudia kukusanya kupitia vyanzo mbalimbali ikiwa ni pamoja na mapato ya ndani,ruzuku kutoka Serikali kuu na fedha za nje kwa ajili ya miradi ya Maendeleo.
Kupitia mapato ya ndani Halmashauri ya Mji Makambako inakusudia kukusanya jumla ya bil. 4.07,ruzuku kutoka Serikali kuu bil. 21.21 na fedha za nje kwa ajili ya miradi ya maendeleo bil. 3.47.
Aidha, Halmashauri ya Mji Makambako inakusudia kutumia kiasi cha bil. 28.75 kwa kila kasma ,ambapo kiasi cha bil. 17.46 , sawa na asilimia 60.8 kwa ajili ya mishahara,bil. 3.59 sawa na asilimia 12.5 ni fedha kwa ajili ya matumizi mengine ya kiutawala na kiutendaji na bil. 7.68 sawa na asilimia 26.7 ni fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa