• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO
HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na maliasili
      • Raslimali watu na Utawala
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Usafi na mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Ujenzi na Uokoaji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Sekondari
      • Kilimo, Ushirika na umwagiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
    • Vitengo
      • Sheria
      • ICT and Public relations
      • Ugavi na Manunuzi
      • Mkaguzi wa ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma ya Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya kumwona Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti mbalimbali
    • Mikataba
    • Mpango Mkakati
    • Hatua
    • Fomu za maombi
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio
    • jarida la mji

Baraza la Madiwani laishauri Serikali juu ya simba wawili waliovamia Makambako.

Tarehe iliyowekwa: July 31st, 2023


Na. Lina Sanga

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Makambako,limetoa ushauri na maoni kwa Serikali juu ya namna ya kuwadhibiti simba hao,ikiwa ni pamoja na kuwatumia wawindaji kutoka  jamii ya wamang’ati , wasaidie kuwawinda simba hao na kufanya  maboresha ya mbinu za utafutaji wa wanyama wanaotoroka maeneo ya hifadhi ili kuwadhibiti mapema kabla hawajasababisha madhara makubwa.

Ushauri na maoni hayo yametolewa leo   katika majadiliano baada ya kuwasilishwa kwa ajenda ya dharura ya uwepo wa simba wawili katika Halmashauri ya Mji Makambako, iliyowasilishwa katika Mkutano wa baraza la madiwani wa kuishia kipindi cha robo ya nne kwa mwaka wa fedha 2022/2023,uliofanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri.

Kwa nyakati tofauti Madiwani wamepongeza na kuishauri Serikali kupitia Wizara ya Maliasili kwa jitihada za kuwatafuta simba hao na kuitaka  kuongeza nguvu zaidi  ya kuwapata simba hao kabla hawajaleta madhara makubwa zaidi ,kwani wananchi wana hofu na shughuli za uzalishaji zimesimama kutokana na uwepo wa simba hao.

Awali akitoa taarifa hiyo Afisa Mazingira na Maliasili wa Halmashauri ya Mji Makambako, Gift Kiwia amesema kuwa,mnamo julai 29,2023 iliripotiwa uwepo wa simba wawili katika Mtaa wa Malombwe,Kata ya Lyamkena waliovamia na kuua ng’ombe 2,julai 30 walivamia na kuua nguruwe 1 na leo julai 31,2023 imeripotiwa uwepo wa simba hao katika Kijiji cha Mkolango,Kata ya Mlowa  baada ya kuvamia na kuua ng’ombe 1 na nguruwe 2.

Ametoa rai kwa wananchi kuendelea kuchukua tahadhali kwani simba hao wanafanya uvamizi hasa nyakati za usiku,hivyo kwa wananchi wenye mifugo wajitaidi kuwasha moto usiku karibu na mazizi ya mifugo na kuwahakikishia kuwa skari 8 kutoka Mamlaka ya Uhifadhi wa Wanyamapori Tanzania(TAWA)wanafanya jitihada za kuwatafuta simba hao na kuwadhibiti.

Naye,Mkuu wa Wilaya ya Njombe,Mhe. Kissa Gwakisa Kasongwa amewataka wananchi wa Halmashauri ya Mji Makambako kuendelea kuchukua tahadhali ,kutokana na uwepo wa simba katika maeneo mbalimbali ndani ya Makambako,na kuwahakikishia kuwa Serikali ipo pamoja nao kwa kuhakikisha simba hao wanatafutwa na kudhibitiwa.

Matangazo

  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 13 April 19, 2025
  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 12. April 20, 2025
  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 11. April 21, 2025
  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 10. April 22, 2025
  • Fungua

Habari Mpya

  • Wataalamu na viongozi watakiwa kusimamia upatikanaji na utoaji wa huduma za chanjo.

    April 25, 2025
  • Makambako yang'ara katika tuzo za Afya ya Usafi wa Mazingira ngazi ya Halmashauri za Miji.

    April 09, 2025
  • Jumla ya Miti 15,000 kupandwa Halmashauri ya Mji Makambako kuelekea siku ya Miti duniani mwaka 2025.

    March 15, 2025
  • Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 2025 Mkoa wa Njombe, Mila kandamizi zaelezwa kuwa kikwazo cha ustawi na uwezeshaji

    March 09, 2025
  • Fungua

Video

Shule mpya ya Mbugani Kitandililo sekondari kupitia mradi wa SEQUIP
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Fursa za Usafirishaji
  • Orodha ya Madiwani
  • Uzalishaji wa Umeme wa Upepo
  • Organisation Structure
  • Fursa za Biashara
  • By Laws
  • Permanent Committee

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu ya Rais
  • Tovuti ya Ofisi ya Utumishi
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Open Data Tanzania

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Makambako Town Council

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako

    Simu ya mezani: 026-2730044

    Simu ya Kiganjani: 0785635383

    Barua pepe: td@makambakotc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa