Na. Lina Sanga
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Makambako limemshukuru Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali pamoja na Waziri wa Kilimo na Mbunge wa jimbo la Makambako Mhe. Daniel Chongolo kwa hatua alizozifanya kwa maendeleo ya jimbo ndani ya muda mfupi tangu aingie madarakani.
Akitoa shukrani hizo leo Mwenyekiti wa baraza hilo,Mhe. Salum Mlumbe amesema kuwa suala la shida ya mtandao katika Mtaa wa Kiumba na Ikelu limedumu kwa muda mrefu lakini kwa sasa kupitia uongozi wa Mhe. Chongolo mafundi wapo wanajenga mnara wa simu katika maeneo hayo ili kutatua changamoto ya mawasiliano iliyolalamikiwa kwa muda mrefu.
“Ndani ya muda mfupi tumeshuhudia kazi kubwa zinafanywa na Mbunge wetu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa minara ya simu Ikelu na Kiumba,lakini pia ameendelea kupeleka michango mbalimbali kwenye maeneo yetu wiki iliyopita tulipeleka bati 100 kwenye shule Fulani pale na ameendeleo kufanya hivyo shule mbalimbali na sasa ametoa gari ya shughuli za maendeleo, wananchi wamjulishe kuhusu shughuli za maendeleo kwenye maeneo yao gari ipo na atajaza mafuta mwenyewe”,alisema Mhe. Mlumbe.
Pia amesisitiza utekelezaji wa maelekezo ya Mkuu wa Wilaya ya Njombe,Mhe. Juma Sweda aliyoyatoa wakati akitoa salamu za Serikali ikiwa pamoja na kuwasaka watoto ambao bado hawajaripoti shuleni,suala la uhifadhi wa mazingira kwa kupanda miti na utoaji wa huduma ya bima ya afya kwa wote.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa