• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO
HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na maliasili
      • Raslimali watu na Utawala
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Usafi na mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Ujenzi na Uokoaji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Sekondari
      • Kilimo, Ushirika na umwagiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
    • Vitengo
      • Sheria
      • ICT and Public relations
      • Ugavi na Manunuzi
      • Mkaguzi wa ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma ya Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya kumwona Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti mbalimbali
    • Mikataba
    • Mpango Mkakati
    • Hatua
    • Fomu za maombi
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio
    • jarida la mji

Baraza la Madiwani limepitisha Rasimu ya Mpango na Bajeti yenye Jumla ya shilingi Bilioni 25.9 Mwaka wa Fedha 2022/2023

Tarehe iliyowekwa: February 18th, 2022

Na. Lina Sanga

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Makambako leo,limepitisha Rasimu ya Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/2023 yenye Jumla ya Shilingi bil. 25.9, ili kuiwezesha Halmashauri ya Mji Makambako  kutekeleza shughuli mbalimbali za kiutalawa na kiutendaji pamoja na utekelezaji wa miradi ya maendeleo na Jumla ya shilingi Mil. 700 ikiwa ni uchangiaji wa nguvu za Wananchi kwenye Miradi ya Maendeleo.

Akiwasilisha Rasimu hiyo Afisa Mipango wa Halmashauri ya Mji Makambako, Bw. Eliud Mwakibombaki amesema kuwa Halmashauri   imeomba kuidhinishiwa kiasi hicho cha fedha,ikiwa shilingi Bil. 15.1 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi, shilingi Bil. 2.6 Kwa ajili ya matumizi mengine na shilingi Bil. 8.2 kwa ajili ya  Miradi ya Maendeleo.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako,Bw. Kenneth Haule amesema kuwa Halmashauri kwa sasa inatarajia kuanzisha miradi mbalimbali ili kuongeza makusanyo ya mapato ya halmashauri ikiwa ni pamoja na kuanzisha maegesho ya malori katika Kata ya Majengo na Mradi wa kufyatua tofali.

Haule amesema kuwa halmashauri inatakiwa kukusanya jumla ya shilingi bil. 2.7 ikiwa ni mapato ya ndani,na mapato hayo yanakusanywa ngazi ya Kata na ngazi ya Halmashauri katika vyanzo vya mapato vinavyotambulika kisheria na sio idadi ya watu waliopo kwenye Kata husika.

“Ukusanyaji wa mapato hauzingatii idadi ya watu bali vyanzo vinavyotambuliwa  kisheria,lakini mgao wa mapato unafanyika kwa kuzingatia idadi ya watu ,hivyo ni wajibu wa kila mwananchi kulipa kodi na ushuru wa mapato wa Halmashauri  kama sheria inavyotaka  na watendaji wa Kata,Mitaa na Vijiji  wanawajibu wa kukusanya mapato ili Bajeti ya Halmashauri iongezeke”,alisema Haule.

Aidha, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako, Bw. Hanana Mfikwa ametoa wito kwa Halmashauri kuendelea kutafuta vyanzo vya mapato,ili kuongeza makusanyo ya mapato ambayo yatasaidia kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa shule na huduma mbalimbali za  kijamii.

Wakati huo huo, Katibu Tawala Wilaya ya Njombe, Bw. George Emmanuel amepongeza Baraza la Madiwani kwa kupitisha Rasimu ya Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2022/2023,lakini pia amewataka wananchi wote wa Halmashauri ya Mji Makambako kujitokeza kushiriki Zoezi la Uwekaji wa Anwani za Makazi,Uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru ambapo kwa mwaka huu utafanyika Mkoa wa Njombe sambamba na zoezi la Sensa za Watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika Mwezi Agosti Mwaka huu Nchi nzima.

Matangazo

  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 13 April 19, 2025
  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 12. April 20, 2025
  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 11. April 21, 2025
  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 10. April 22, 2025
  • Fungua

Habari Mpya

  • Wataalamu na viongozi watakiwa kusimamia upatikanaji na utoaji wa huduma za chanjo.

    April 25, 2025
  • Makambako yang'ara katika tuzo za Afya ya Usafi wa Mazingira ngazi ya Halmashauri za Miji.

    April 09, 2025
  • Jumla ya Miti 15,000 kupandwa Halmashauri ya Mji Makambako kuelekea siku ya Miti duniani mwaka 2025.

    March 15, 2025
  • Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 2025 Mkoa wa Njombe, Mila kandamizi zaelezwa kuwa kikwazo cha ustawi na uwezeshaji

    March 09, 2025
  • Fungua

Video

Shule mpya ya Mbugani Kitandililo sekondari kupitia mradi wa SEQUIP
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Fursa za Usafirishaji
  • Orodha ya Madiwani
  • Uzalishaji wa Umeme wa Upepo
  • Organisation Structure
  • Fursa za Biashara
  • By Laws
  • Permanent Committee

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu ya Rais
  • Tovuti ya Ofisi ya Utumishi
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Open Data Tanzania

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Makambako Town Council

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako

    Simu ya mezani: 026-2730044

    Simu ya Kiganjani: 0785635383

    Barua pepe: td@makambakotc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa