Na. Lina Sanga
Njombe
Rai hiyo imetolewa leo na Katibu Tawala Mkoa wa Njombe Bi. Judica Omari,wakati akifungua semina kwa watumishi wa Umma Mkoani Njombe juu ya uwekezaji kwenye dhamana za Serikali inayotolewa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) tawi la Mbeya,katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe.
Amesema mafunzo hayo yamekuja kwa wakati muafaka na yana tija kwa ustawi wa uchumi wa watumishi wote hivyo BOT hawana budi kuandaa ratiba mahsusi ya mafunzo hayo,ili kuwafikia watumishi wote wa Mkoa wa Njombe na Mikoa mingine.
Amewataka washiriki wa semina hiyo kusikiliza kwa umakini kutokana na umuhimu wa mafunzo hayo ,ambayo yatawawezesha kuwekeza kwenye dhamana za Serikali kwani ni salama na kujipatia faida na kuiwezesha Serikali kuongeza mapato.
Agathon Kipandula, Meneja fedha na utawala Benki Kuu ya Tanzania(BOT) tawi la Mbeya amewataka watumishi wa Umma kufanya uwekezaji huo kwa tija na kutohofia uvumi unaotolewa, kwani katika dunia kuadimika kwa dola hutokea nchi zote duniani na sio Tanzania pekee.
Amesema kuwa,BOT inafanya kazi kwa niaba ya Serikali kuuza dhamana za Serikali ,kwa njia ya minada ikiwa ni njia mojawapo ya kukopa fedha katika soko la ndani, kwa uwekezaji wa muda mrefu na mfupi kupitia mfumo wa masoko wa soko la awali na soko la upili bila kuathiri mikopo kwa sekta binafsi.
“Katika soko la awali BOT huuza dhamana za Serikali kwa mnada kila wiki siku ya jumatano kwa njia ya ushindani na isiyo ya ushindani, ambapo kila mkazi wa jumuiya ya Afrika mashariki anastahili kushiriki na soko la upili uuzaji hufanyika na wawekezaji wenyewe”,alisema Agathon.
Washiriki wa Semina hiyo ni Wakuu wa Idara,Vitengo na Sehemu ngazi ya Mkoa na Halmashauri pamoja na taasisi za Serikali Mkoani Njombe.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa