Pichani ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Paulo Malala na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Makambako Hanana Mfikwa kwa furaha wakiwaonesha Madiwani wa Halmshauri ya Mji wa Makambako Cheti kilichotolewa na Bodi ya wahasibu na wakaguzi wa hesabu za Tanzania(NBA) katika ufungaji bora wa hesabu kwa Mamlaka za serikali za mitaa, ambapo kwa mwaka 2019 ilishika nafasi ya kwanza kitaifa na kwa mwaka 2020 kwa nafasi ya pili kitaifa katika zoezi zima la ufungaji wa hesabu za Serikali kwa mamlaka za serikali za Mitaa. Zoezi la kuonesha Baraza la Madiwani limefanyika katika kikao cha Baraza la Madiwani Mnamo tarehe 17,02,2021 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa