Na. Lina Sanga
Ili kukabiliana na changamoto ya ukosefu wa ajira kwa vijana,Halmashauri ya Mji Makambako inatarajia kujenga chuo cha ufundi stadi(VETA),ili vijana waweze kujiendeleza na baadaye kujiajiri na eneo la ujenzi wa chuo hicho limeshapatikana.
Hayo yameelezwa na Mbunge wa Jimbo la Makambako, Mhe. Deo Sanga katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo katika kitongoji cha Nyambogo,Luhota na Kijiji cha Ngamanga,Kata ya Utengule ikiwa ni ziara ya Mbunge ya kijiji kwa kijiji,Mtaa kwa Mtaa ili kuongea na wananchi,kusikiliza kero zao na kutoa jumbe mbalimbali za Serikali ikiwa ni pamoja na Ujumbe wa Sensa ya watu na Makazi 2022,Mbolea ya ruzuku na bajeti ya Serikali ya mwaka 2022/2023.
Amesema kuwa kutokana na changamoto ya ajira nchini,chuo cha VETA kitawawezesha vijana wanapohitimu elimu ya msingi,kidato cha nne na kuendelea,kujiunga na chuo hicho kujifunza kazi mbalimbali ili waweze kujiajiri badala ya kusubiri kuajiriwa,kwani Serikali imeshaweka utaratibu wa utoaji mikopo ya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ili kuwawezesha vijana kupata mtaji wa kuanza biashara au kilimo na shughuli nyingine.
Pia,amempongeza uongozi wa kijiji cha Ikelu kwa kujitoa kuchangia ujenzi wa Kituo cha Afya,nyumba ya watumishi pamoja na shule ya msingi shikizi Ikelu B,yenye maboma matano na ofisi Moja na darasa moja limekamilika kwa fedha ya ruzuku kutoka Serikali Kuu shilingi Mil. 12.5 na darasa hilo linaweza tumika ili kuwapunguzia wanafunzi umbali wa kutembea hadi shule ya Msingi Ikelu.
Aidha,ametoa wito kwa viongozi wa dini kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhakikisha Tanzania inapata maendeleo,na Halmashauri ya Mji Makambako pia kwa kutoa fedha za miradi na maendeleo.
Pia,ametoa wito kwa wazee vijiji kuwaombea Mhe. Samia pamoja na Viongozi wote wa Mji wa Makambako,kwa sababu mila zipo na Serikali inawaamini.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa