Na. Tanessa Lyimo
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe.Juma Sweda amewataka wananchi wa Mtaa wa Mashujaa katika Kata ya Kivavi na Mtaa wa Majengo,katika Kata ya Majengo kuwa na subira, wakati akifatilia na kufanya mazungumzo na Kampuni ya SINOTAN inayojishughulisha na ufuaji umeme wa upepo, kuhusu madai ya fidia baada ya wananchi kuachia maeneo yao ili kupisha utekelezaji wa mradi huo.
Mhe. Sweda alitoa kauli hiyo jana katika mkutano wa hadhara katika Kata hizo, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kusikiliza na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili wananchi katika Halmashauri ya Mji Makambako.
Aidha, ametoa wito kwa viongozi wa dini kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya ukatili wa kijinsia na kuwataka wananchi kuwafichua wahalifu katika jamii inayowazunguka.
Ametoa rai kwa waratibu wa elimu Kata kuhakikisha bustani za Mbogamboga zinapandwa shuleni, ili kuhakikisha wanafunzi wanapata lishe bora ili kukabiliana na udumavu.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa