Na. Lina Sanga
Rai hiyo ilitolewa jana na Kamati ya Siasa Wilaya ya Njombe, walipotembelea shule ya Msingi Mfumbi kujagua nyumba pacha ya walimu,ikiwa ni ziara ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji Makambako kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Akizungumza na Viongozi wa ngazi ya Kata na Halmashauri,Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Wilaya ya Njombe,Mhe. Justin Nusulupila Sanga amepongeza ujenzi wa nyumba ya kisasa kwa ajili ya walimu pamoja na ujenzi wa shule hiyo na kuwapunguzia mwendo wanafunzi kutembea zaidi ya kilomita 10 kila siku hadi shule ya msingi Kitandililo.
Amesema kuwa ujenzi wa shule hiyo yenye wanafunzi 78 kwa sasa na nyumba za walimu, una manufaa makubwa kwa wananchi wa Kitongoji cha Mfumbi,kwani kwa muda mrefu hawakuwa na shule ya msingi hivyo kuna baadhi ya watu wazima, huenda walikosa nafasi ya kujiunga na shule kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na utoro,hivyo ni wakati sahihi kwa Halmashauri kutoa elimu ya watu wazima kwa waliyoikosa.
Aidha Kamati hiyo ilitembelea mradi wa ujenzi wa jengo la wagonjwa wa dharura(EMD), katika Hospitali ya Mji iliyopo Mlowa,na kuishukuru Serikali kwa kutoa vifaa vya kisasa kwa ajili ya huduma ambazo zilikuwa zinatolewa Hospitali kubwa.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa