Na. Lina Sanga
Rai hiyo imetolewa leo na Mkuu wa divisheni ya Maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya Mji Makambako, Bi. Lilian Mwelupungwi wakati akifungua mafunzo kwa vikundi 81 vya Wanawake 57, Vijana 14 na watu wenye ulemavu 10 ambavyo vimenufaika na mikopo ya asilimia 10 awamu ya kwanza inayotolewa na Halmashauri na jumla ya mil. 474.9 zimetolewa.
Bi. Mwelupungwi amesema kuwa, wahitaji wa mikopo hiyo ni wengi hivyo waliopata mkopo kwa awamu ya kwanza,hawana budi kuhakikisha wanatumia fedha walizopata kutekeleza shughuli walizoombea mikopo ili marejesho yarejeshwe kwa wakati na wahitaji wengine wa mikopo hiyo waweze kunufaika.
“ombi langu lile lile la awali muende mkafanyie kazi shughuli zile ambazo mmeziombea ili mwisho wa siiku marejesho yarejeshwe, mtakaporejesha nyinyi kwa wakati hata wale ambao kwa awamu hii wamekosa tunaamini wataenda kupata, naomba tuwe tayari kwa mafunzo haya”,alisema Mwelupungwi.
Baadhi ya wenyeviti wa vikundi vya wanawake,vijana na watu wenye ulemavu katika Kata ya Mjimwema Bi.Maria Kalua na Bi.Agape Joackim pamoja na Bw. Sumbuko Sanga ambaye ni mlemavu, wameishukuru Serikali kwa kutoa mikopo hiyo kwa wajasiriamali ili kuwawezesha wajasiriamali hao kuondokana na tatizo la ukosefu wa mitaji ya biashara na kuahidi kusimamia vikundi kwa weledi kwa kuhakikisha kila mnufaika anatumia mkopo kwa shughuli aliyoombea mkopo ili aweze kufanya marejesho kila mwezi na kumaliza mkopo kwa wakati ili na wengine wanufaike kama wao.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa