Na. Lina Sanga
Rai hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Njombe Mhe. Justin Nusulupila Sanga ,katika ziara ya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa usambazaji maji Kata ya Mlowa, katika Halmashauri ya Mji Makambako chini ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Makambako (MAKUWASA).
Mhe. Sanga amesema kuwa, mita za maji za malipo ya kabla (luku) ni suluhisho la kumaliza malalamiko ya watumiaji maji ya kuzidishiwa bili, kwani mtumiaji atatumia maji kwa kiasi cha fedha alicholipa kama ilivyo kwa watumiaji wa umeme.
“TANESCO wamefanikiwa kumaliza malalamiko ya kuzidisha bili ya umeme kwa wateja,hivyo hata MAKUWASA mnaweza kumaliza malalamiko kupitia mita za malipo ya kabla kwani mwananchi atatumia kiasi cha maji alicholipia”,alisema Mhe. Sanga.
Awali akiwasilisha taarifa ya ujenzi wa mradi huo Clement Malumwene kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa MAKUWASA, amesema kuwa mradi huo unaogharimu Bil. 3.5 ,kwa sasa umekamilika kwa asilimia 80 na utaunganishwa kupitia mradi wa maji wa Miji 28 ili wananchi wa Mlowa waweze kupata huduma ya maji iliyokosekana kwa muda mrefu.

Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Njombe imetembelea jumla ya miradi sita katika Halmashauri ya Mji Makambako ikiwa ni pamoja na ujenzi wa daraja la mawe barabara ya Muungano Kata ya Utengule,mradi wa madarasa 3 na matundu 7 ya vyoo shule ya msingi Lyamkena,kutembelea shughuli za kikundi cha Vijana RAJISFAT Mtaa wa Magegele,Kata ya Kivavi,ujenzi wa shule Moya ya sekondari ya Mjimwema Mtaa wa Igangidung’u,Kata ya Kivavi na ujenzi wa zahanati ya Mwembetogwa katika Kata ya Mwembetogwa.




Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa