Na. Lina Sanga
Kauli hiyo imetolewa na Afisa mifugo wa Halmashauri ya Mji Makambako,Samora Mgaya katika Mkutano wa baraza la Madiwani la kipindi cha kuishia robo ya tatu 2022/2023,uliofanyika juni 6,2023 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Makambako.
Mgaya alitoa kauli hiyo wakati akijibu hoja ya diwani wa Kata ya Mwembetogwa,Mhe. Oddo chaula kuhusu tetesi za uwepo wa ugonjwa wa homa ya nguruwe katika Mji wa Makambako baada ya Wilaya ya Ludewa na Makete kutangaza zuwio la ulaji wa nyama ya nguruwe kutokana na uwepo wa ugonjwa huo.
Amesema kuwa,Halmashauri ya Mji Makambako ilikumbwa na ugonjwa wa homa ya nguruwe kabla ugonjwa huo kutangazwa katika Wilaya za jirani, na wataalamu wa mifugo kwa kushirikiana na wizara walifanikiwa kuudhibiti mapema na kuutokomeza kabisa na sasa hali ni shwari.
Amewatoa hofu walaji wa nyama ya nguruwe kuendelea kula nyama hiyo bila hofu,kwani endapo kama ugonjwa huo ungekuwepo tamko la zuio la uuzaji na ulaji wa nyama ya nguruwe lingetolewa.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako,Mhe. Hanana Mfikwa ametoa rai kwa Madiwani,Viongozi na wananchi kutosikiliza taarifa zisizo rasmi zinazosambaa mitaani kuhusu mambo mbalimbali,ikiwa ni pamoja na uwepo wa magonjwa ya mifugo kwani wasemaji wa masuala husika wapo na wana mamlaka ya kutoa taarifa sahihi kwa Umma.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa