Na. Lina Sanga
Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango miji na mazingira,Mhe. Navy Sanga ametoa rai kwa wananchi wa Halmashauri ya Mji Makambako,kuendelea kulipa ada ya uzoaji taka kwa kila kaya na sehemu ya biashara,kwani hakuna mwananchi asiyezalisha taka.
Mhe. Navy alitoa rai hiyo juni 6,mwaka huu katika Mkutano wa baraza la Madiwani la kipindi cha kuishia robo ya tatu 2022/2023,uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Makambako.
Amesema kuwa,kupitia kamati ya Mipango Miji na Mazingira wamebaini uwepo wa wananchi wanaokwepa kulipa ada ya uzoaji taka katika kaya,maeneo ya biashara na taasisi binafsi na kuikosesha Halmashauri mapato kwa ajili ya utekelezaji wa zoezi la uzoaji taka na kuweka Mji katika hali ya usafi.
Ametoa wito kwa wananchi wote kujenga tabia ya kupenda usafi wa mazingira wanayoishi na kuacha tabia ya kutupa taka ovyo barabarani na mitaroni,ili kuuweka Mji katika hali ya usafi na kuepukana na magonjwa ya mlipuko.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa