Na. Lina Sanga
Mhe. Imani Fute kwa niaba ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako na Madiwani wote,ametoa kauli hiyo leo Katika hafla ya uzinduzi wa Miongozo ya elimu ngazi ya Halmashauri, uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Mji Makambako.
Akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya fedha na Uongozi,Maafisa elimu idara ya Msingi na Sekondari,Wakuu wa shule na Walimu wakuu wote pamoja na wanafunzi ,Mhe. Fute amesema kuwa ipo haja ya walimu kuwashirikisha madiwani ili kufikia lengo la kukuza taaluma katika Kata zote za Halmashauri ya Mji Makambako.
Mhe. Fute amesema kuwa,Serikali chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanya vizuri katika eneo la elimu hasa kwenye uandaaji wa miongozo ya uboreshaji elimumsingi na sekondari pamoja na mkakati wa kuimarisha ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya elimumsingi.
Ameongeza kuwa,ipo haja ya Walimu kuwashirikisha Madiwani katika utekelezaji wa jambo lolote linalofaa ili kukuza taaluma,kwani Madiwani pia wana nia njema ya kuhakikisha taaluma katika Halmashauri hiyo inapewa kipaumbele na inaendelea kukua kila siku.
Amesema ili taaluma iendelee kukua ipo haja ya kila mtu kusimama vizuri katika nafasi yake, kuanzia wananchi,madiwani na walimu, na diwani ni kiungo muhimu kati ya wananchi na walimu kwani wanatoka miongoni mwa wananchi wa Kata husika.
Ametoa wito kwa walimu kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi,kwa kutambua madiwani wote wana nia njema na wanawapenda kwani wanatambua kazi kubwa na jitihada zao wanazozifanya katika kuhakikisha taaluma inakua.
Vitabu vya miongozo vilikabidhiwa kwa Afisa elimu taaluma Halmashauri ya Mji Makambako na Mratibu elimu Kata kwa ajili ya kuuanza utekelezaji.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa