Na. Lina Sanga
Halmashauri ya Mji Makambako katika kipindi cha robo ya pili katika mwaka wa fedha 2022/2023,imefanikiwa kutoa mikopo ya asilimia 10 kupitia mapato ya ndani jumla ya mil 76 kwa vikundi 12 vya wanawake na vijana na watu 8 wenye ulemavu.
Akizungumza na wana vikundi hao katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Mji Makambako,Mhe. Hanana Mfikwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako amewapongeza vijana walipata mkopo katika awamu ya pili na kuwataka kutimiza malengo waliyojiwekea badala ya kugawanyika baada ya kukabidhiwa mikopo.
“Vijana wengi mnajitahidi sana kujishughulisha na kuunda vikundi kwa ajili ya kupata mkopo,lakini vijana wengi baada ya kupata mikopo hutawanyika na kuvunja kikundi hali inayosababisha marejesho kusua sua na wengine hutoroka kabisa baada ya kupata mikopo,hivyo kila mmoja aliyepo humu na amepata mkopo ajitahidi kutunza uaminifu ili na wengine wanufaike kupitia fedha hizi zinazotolewa na Serikali.
Ametoa wito kwa wanufaika wote wa mikopo hiyo kutumia fedha hizo kutumia fedha hizo katika malengo yaliyokusudiwa,badala ya kununua mavazi,kutoa michango ya sherehe ambazo haziwezi kuwaongezea kipato kitachowawezesha kulipa marejesho na kuongeza kipato chao.
Jumla ya watu 8 wenye ulemavu wamepata Mkopo,Vikundi vya vijana 3 ambapo kikundi kimoja kimepata mkopo wa bajaji na vikundi 9 vya wanawake wanaojishughulisha na ujasiriamali,kilimo cha viazi na ufugaji wamepata mkopo.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa