Na. Lina Sanga
Kauli hiyo imetolewa leo na Msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri ya Mji Makambako, Ndg. Kenneth Haule katika kikao cha kupitia ratiba za kampeni ya uchaguzi na viongozi wa vyama vya siasa kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya MjI Makambako huku akiwataka viongozi hao kuwa wasikilizaji zaidi badala ya kuwa waongeaji.
Haule amesema kuwa, sifa ya kiongozi ni kuwa na masikio makubwa ya kusikiliza, macho makubwa ya kuangalia, pua kubwa ya kunusa mambo mbalimbali na mdomo mdogo ili aweze kupata nafasi ya kusikiliza zaidi kuliko kuongea kwani kazi ya kiongozi ni kuongoza njia na wananchi wanawasikiliza sana.
Ametoa rai kwa vyama vya siasa kudhibiti munkari wakati wa kampeni na kuwapa wananchi nafasi ya kufanya maamuzi yao wakati wa uchaguzi kwani hata baada ya Uchaguzi Makambako lazima iwepo na maisha lazima yaendelee.
Amewashukuru viongozi wa vyama vya Siasa katika Halmashauri ya Mji Makambako kwa ushirikiano na ushiriki wao tangu mchakato wa uchaguzi uanze,na kuwaomba ushirikiano huo uendelee ili Makambako isiwe mfano mbaya katika Taifa la Tanzania.
Naye,Mkuu wa polisi Wilaya ya Kipolisi Makambako, ODC Omary Diwani amevitaka vyama vya Kisiasa kuzingatia ratiba iliyokubaliwa,ili kuepusha migogolo isiyo ya lazima.
Viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria kikao hicho France Kinyamagoha wa ACT wazalendo, Benedicto Kyando ,Mwenyekiti wa CHADEMA na Asha Madege,Katibu wa CCM Kata ya Maguvani wamesema kuwa wapo tayari kushiriki kampeni ya uchaguzi kwa kuzingatia kanuni na miongozo na kutoa rai kwa wananchi kujitokeza kwenye mikutano ya kampeni kusikiliza sera za vyama hivyo.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa