Na. Lina Sanga
Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako, Mhe. Hanana Mfikwa katika mkutano wa baraza la Madiwani la robo ya kwanza katika mwaka wa fedha 2023/2024.
Mhe. Hanana ametoa kauli hiyo mara baada ya mjumbe wa baraza hilo kuhoji namna gani Halmashauri ya Mji Makambako imejipanga kupata eneo la kutupa taka, mara baada ya baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe kutoa tamko la kupinga matumizi ya dampo la Itengelo,lililopo Kata ya Saja kupitia vyombo vya habari.
Mhe. Hanana amesema kuwa, Halmashauri haifanyii kazi vyombo vya habari bali vikao, na vyombo vya habari vinatoa taarifa za vikao na Halmashauri ya Mji Makambako haina katazo lolote la kutupa takataka kwenye dampo la Itengelo bali ruhusa ya kutupa taka kwenye eneo hilo na Halmashauri ya Wilaya ya Wanging'ombe ambao ndiyo wenye eneo wanajua na wana barua yenye ruhusa inayowataka kuipa Halmashauri ya Mji Makambako ushirikiano kuhusu kutupa taka kwenye eneo hilo.
" Sisi kama Halmashauri hatuna katazo lolote la kutupa takataka kwenye eneo lile bali tuna ruhusa ya kutupa takataka kwenye eneo lile na linafaa kutupa takataka, na wao wenye eneo hilo wanajua na wana barua inayoturuhusu sisi na inayowataka wao kutupa ushirikiano sisi kuhusu kutupa taka kwenye eneo lile kwa hiyo hii ndiyo taarifa na ndiyo habari", alisema Mhe. Hanana.
Aidha, amesema kuwa wakati muafaka utakapofika wa kuwa na eneo mbadala kwa kadri ya mahitaji,zoezi la kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na eneo la kutupa taka linafanyiwa kazi na watendaji kama ambavyo maandalizi mengine yanavyofanyika kama ujenzi wa madarasa, nyumba,barabara na miundombinu mingine.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa