Ni kikao cha baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji wa Makambako ambacho hufanyika kila baada ya miezi mitatu lengo likiwa ni kujadili mapato na matumizi pamoja na miradi ya maendeleo ya Halmashauri. Katika kikao hicho masuala mbalimbali muhimu ambayo yamejadiliwa ni pamoja na :
Ukusanyanji wa mapato ya Halmashauri ambapo imejadiliwa kuwa mapato kwa sasa si yakuridhisha hivyo basi watendaji /wahusika wa kuhimiza na kufuatilia suala la mapato ni vema wakashirikiana kwaajili ya kuongeza mapato ya Halmashauri kwa maendeleo kwa ujumla.
Suala la elimu kwa shule za Msingi na sekondari pia wazazi wamahimizwa kuendelea kuchangia chakula cha mchana kwa wanafunzi ili kuboresha mazingira ya elimu lakini pia Kuchangia madawati kwaajili ya watoto wao lengo likwa ni kuepusha adha ya watoto kukosa viti na madawati.
Suala la usalama kwa Halmashauri ,ambapo kamati ya Ulinzi na usalama imewahakikishia wajumbe kuwa hali ni shwari lakini suala la ushirikiano kwa wajumbe hususani Madiwani ,Wananchi na Watendaji katika masuala mazima ya kuwafichua wale wanao ashiria vitendo vya kuvunja amani na usalama wa Halmashauri kwa ujumla .
Miundo mbinu ya barabara bado imetizamwa kwa jicho la tatu kwani barabara nyingi zimeharibiwa hasa katika msimu wa masika hivyo zinatakiwa kufanyiwa marekebisho makubwa hasa kwa barabara za pembezoni mwa Mji mfano:Maguvani ,Mtanga,Mahongole na usetule barabara hizo zipo katika kiwango ambacho Tarura wanatakiwa kufanyia kazi kwani ni mbovu kwaujumla .
Suala la maji pia Baraza limejadili kwa kina kwa kata za Halmashauri ya Mji wa Makambako, bado kata ya Mlowa ina changamoto kubwa sana ya maji hasa ukizingatia uwepo wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Makambako yenye hadhi ya Wilaya hivyo umuhimu wa maji maeneo hayo ni mkubwa sana ,aidha maeneo ambayo yanapata huduma ya maji ya bomba bado changamoto yake ni kubwa,kwani maji hutoka machafu jambo ambalo wajumbe wametaka mamlaka husika kujibia suala la maji kutoka katika hali ya rangi ya matope ambapo majibu yake yamejibiwa kuwa zoezi la kutibu maji linaendelea kwaajii ya Wananchi kupata maji safi .
Pia waheshimiwa Madiwani wamependekeza kuwa maeneo ya wazi katika Halmashauri ya Mji wa Makambako yasiachwe kwa muda mrefu sana yafanyiwe kazi ambapo wajumbe wameshauri kuwa ni vema eneo la wazi la stendi ya maroli Mwembetogwa ianzishwe hata bustani ambayo itakuwa kama kivuto cha utalii na kuongeza mapato ya Halmashauri ya Mji wa Makambako.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa