Na. Lina Sanga
Njombe
Wakuu wa mikoa ya ukanda wa Kusini mwa Tanzania,wakuu wa wilaya pamoja na wasaidizi wote,wamekiri kuwa tayari kuibua na kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo katika Mikoa hiyo ili kuendelea kuvutia watalii wengi zaidi kutembelea ukanda huo.
Akizungumza kwa niaba ya wakuu wa Mikoa ya Kusini,Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Zainabu Telack katika hafla ya uzinduzi wa mikakati ya kutangaza utalii kusini mwa Tanzania,iliyofanyika leo katika Ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji Njombe.
Mhe. Telack amesema kuwa,wanazitambua rasilimali kubwa za utalii ambazo Mwenyezi Mungu amejalia ukanda wa kusini,hivyo ni wakati wa Mikoa ya Kusini sasa kuziibua na kuzitangaza rasilimali hizo ili kuongeza idadi ya watalii na kukuza uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
Aidha ametoa shukurani kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuamua kuwekeza kwenye utalii na mambo mengine kwenye nchini, kwa nia ya dhati ya kukuza uchumi wa mtanzania mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kupitia rasilimali mbalimbali zilizopo nchini.
Ametoa wito kwa wadau wanaojishughulisha na utalii kuwekeza katika Mikoa ya Kusini,kwani wameweka Mikakati thabiti ya kukuza utalii kila mkoa ili kuhakikisha utalii unakuwa sehemu ya wananchi kujipatia kipato na kukuza pato la taifa.
Baadhi ya Wakuu wa mikoa waliohudhuria Uzinduzi huo ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Morogoro, Rukwa, Lindi na Njombe ambaye ni mwenyeji wa uzinduzi huo.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa