Halmashauri ya Mji Makambako imeshika nafasi ya pili Kwa upande wa Halmashauri za Miji , katika mashindano ya Kitaifa ya afya ya usafi wa mazingira ikifuatiwa na Halmashauri ya Mji ya Mafinga iliyoshika nafasi ya tatu huku Halmashauri ya Mji Njombe ikishika nafasi ya kwanza.
Akizungumza katika ugawaji wa tuzo hizo zilizofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete katika kilele Cha wiki ya Afya Kitaifa jijini Dodoma, Mganga Mkuu wa serikali ,Dkt. Grace Magembe amewapongeza washindi wote walioshinda tuzo hizo na kuwataka kuendelea kuzingatia usafi na kuhamasisha usafi wa mazingira katika maeneo Yao.
Kwa upande wa Mikoa, Mkoa wa Njombe umeshinda tuzo ya mshindi wa jumla na kupata zawadi ya gari yenye thamani ya Mil. 168 huku washindi wengine wakipata zawadi za vyeti na hundi za fedha.
Wiki ya Afya ilianza Aprili 3,mwaka huu na kilele chake ni Aprili 8,2025 ikiongozwa na kauli mbiu isemayo “Tulipotoka , Tulipo, Tunapoelekea,Tunajenga Taifa Imara lenye Afya”.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa