Na. Lina Sanga
Uongozi wa Halmashauri ya Mji Makambako umetoa wito kwa wamiliki wa mashine za kusaga sembe, kununua viwanja vilivyotengwa na Halmashauri kwa ajili ya viwanda vidogo eneo la majengo na Idofi,ili kuanza ujenzi kabla ya agizo la kuhama halijatolewa.
Mhe. Hanana Mfikwa, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako amesema kuwa, kama walivyohamishwa wenye mashine za kukoboa mpunga muda wa kuhamisha mashine za kusaga sembe pia utafika, hivyo ni wakati sasa kwa wamiliki wa mashine za kusaga sembe kununua viwanja mahususi kwa ajili ya viwanja vilivyotengwa na Halmashauri.
Ametoa wito kwa wamiliki wa mashine hizo kufika katika ofisi ya mkurugenzi ili wapewe maeneo kwa ajili ya ujenzi wa mashine za kusaga sembe na wakabidhiwe hati baada ya kukamilisha malipo , lakini pia Halmashauri itatenga eneo kwa ajili ya kiwanda cha kuzalisha sembe katika eneo la Kiumba ili mtu akinunua mahindi asage sembe papo hapo.
Ametoa rai kwa wafanyabiashara wa mazao wote walio nje ya soko kuu kuhamisha mazao yote soko la kiumba ndani ya siku saba kuanzia leo julai 15,2024 na magari ya mizigo ya viazi kuanza kushusha viazi katika soko la Magegele na Matunda katika soko la Maguvani zaidi ya hapo mfanyabiashara au dereva wa gari litalokamatwa atalazimika kulipa faini isiyopungua Mil. 1.
Leo julai 15,2024 kimefanyika kikao cha timu ya menejimenti na wafanyabiashara wajenzi wa maghala na vizimba katika soko la mazao la Kiumba,kukubaliana muda wa kurejea sokoni ambapo siku saba zimetolewa kwa wafanyabiashara hao kurejea soko rasmi la mazao la Kiumba,magari ya mizigo ya viazi kuanza kushusha viazi soko la Magegele na magari ya mizigo ya matunda kushusha matunda katika soko la Maguvani.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa