Na. Lina Sanga
Mbeya
Mhe. Samia Suluhu Hassan afungua rasmi mfumo wa mbolea ya ruzuku.
Ufunguzi wa mfumo wa mbolea ya ruzuku umefunguliwa rasmi leo na Mhe. Samia Suluhu Hassan,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika viwanja vya John Mwakangale katika kilele cha maadhimisho ya maonyesho ya nanenane Mkoani Mbeya.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa zoezi la mbolea ya ruzuku,Mhe. Hussein Bashe Waziri wa Kilimo amesema kuwa hadi sasa Mfumo umekamilika, kuanzia mbolea inavoingia, usajili wa mbolea,mzabuni na Msambazaji wa mbolea na kuwapa namba za utambulisho.
"Kila mfuko wa mbolea utakuwa na namba yake ambayo haitaweza kutumika tena ,na kila kampuni itakuwa na namba yake,msambazaji atakuwa na namba yake ya utambulisho na kila mkulima atakua na namba yake ya utambulisho",alisema Mhe. Bashe.
Mhe. Bashe amesema kuwa kupitia namba ya utambulisho ya kila mfuko wa mbolea, ukinunuliwa dukani utasomeka kwenye mfumo kwa kuonyesha namba ya mfuko wa mbolea iliyonunuliwa,jina la muuzaji na namba ya utambulisho,mahali ambapo mbolea hiyo imenunuliwa na jina la mkulima na namba yake ya utambulisho.
Amesema suala la usajili wa wakulima na utoaji wa mbolea ya ruzuku kwa sasa umefanyika sambamba kutokana na dharura,lakini baada ya miaka miwili wakulima wote watakuwa wamesajiliwa.
Mhe. Bashe amebainisha bei za ruzuku kwa kila mbolea ambapo mbolea ya DAP inayouzwa 131,000 sasa itauzwa 70,000 bei ya ruzuku mfuko mmoja,mbolea ya UREA inayouzwa 124,734 itauzwa 70,000 bei ya ruzuku kwa mfuko mmoja,Mbolea ya CAN inayouzwa 108,156 itauzwa 60,000 bei ya ruzuku kwa mfuko mmoja,mbolea ya SA inayouzwa 82,852 itauzwa 50,000 bei ya ruzuku kwa mfuko mmoja na mbolea zote za kupandia (NPK) zinazouzwa 122,995 zitauzwa 70,000 kwa mfuko mmoja.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa