Na. Lina Sanga
TASAF kupitia Mfuko wa maendeleo ya jamii miradi yakupunguza umasikini( TPRP IV) kwa mwaka wa fedha 2021/2022 umetoa zaidi ya Mil. 134 , ambazo zimetumika katika ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa na ofisi moja,pamoja na ujenzi wa matundu 12 kwa ajili ya wanafunzi na walimu.
Geofrey Danda,Mwalimu Mkuu wa Shule ya msingi shikizi Magongo iliyopo ,Kata ya Makambako amesema kuwa kupitia madarasa yaliyojengwa kwa ufadhili wa TASAF msongamano wa watoto katika shule ya msingi Juhudi ambayo inatumika hivi sasa utapungua, kwani kwa sasa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1,397 na uandikishaji wa darasa la awali unaendelea.
Amesema kuwa,ujenzi wa madarasa hayo pamoja na vyoo umesaidia kupunguza jumla ya wanafunzi 188 ambao ni kuanzia darasa la kwanza hadi darasa la saba,na msomo yataanza rasmi januari,2023,kwani TASAF imekamilisha miundombinu yote muhimu kuanzia vyoo,madarasa hadi samani ikiwa ni pamoja na madawati,meza,viti na makabati na uandikishaji wa darasa la awali umeanza shuleni hapo.
Ameipongeza Serikali kupitia Mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF) kwa kujenga miundombinu ya madarasa katika shule ya msingi shikizi ya Magongo, ambayo yatasaidia kuongeza mahudhurio ya wanafunzi na kuongeza ufanisi wa ujifunzaji na ufundishaji kwa wanafunzi kutotembea umbali mrefu.
“Hali ya kijiografia katika Mtaa huu wa Magongo kuna mabonde na milima mingi ambayo kwa namna kubwa imechangia mahudhurio hafifu kwa wanafunzi,kila siku mtoto alilazimika kutembea umbali wa kilomita 7 kutoka Magongo hadi shule ya msingi Juhudi iliyopo Mtaa wa Kipagamo,wanafunzi wengine waliishiakwenye vichaka na kukosa masomo kwa sababu ya utoro,kupitia ujenzi wa madarasa haya naamini mahudhurio yatakuwa ya kuridhisha na wanafunzi watapata nafasi ya kujifunza”,alisema Mwl. Danda.
Ametoa wito kwa wazazi na walezi wote katika Mtaa wa Magongo na maeneo jirani,kuwasimamia watoto na kuhakikisha wanahudhuria masomo kila siku kwani Serikali imesogeza huduma ya shule jirani ili watoto wote wapate nafasi ya kujifunza na kukuza taaluma.
Madarasa matano na Ofisi moja yaliyojengwa na Tasaf kwa awamu ya kwanza na awamu ya mili 2021/2022. Vyumba vya Madarasa matatu awamu ya pili katika hatua ya ukamilishaji.
Vyumba vya madarasa mawili na ofisi moja -awamu ya kwanza ujenzi umekamilika.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa