Na. Lina Sanga
Jumla ya Mil. 583.2 zimepokelewa kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika Mtaa wa Idofi, Kata ya Mlowa ili kuwapunguzia mwendo wanafunzi wa Kata hiyo na maeneo ya jirani.
Bw. Nakembetwa Makala, Kaimu Afisa Mipango wa Halmashauri ya Mji Makambako alitoa taarifa hiyo jana, katika hafla ya kutambulisha mradi huo, iliyofanyika katika shule ya Msingi Idofi.
Makala, amesema kuwa fedha hizo zitatekeleza ujenzi wa miundombinu ya madarasa, ofisi, jengo la utawala,vyoo, kichomea taka, maktaba pamoja na maabara za kemia,biologia na fizikia.
Mhe. Odillo Fute, diwani wa Kata ya Mlowa ameishukuru Serikali kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo, na kuwataka wananchi wa Kata hiyo kuupokea mradi na kushiriki kwa kufanya kazi ambazo zinahitaji nguvu ya wananchi kama kusafisha eneo na kuchimba mashimo ya vyoo.
Naye, Katibu wa CCM Kata ya Mlowa, Bw. Ezekiel Chongolo pamoja na wananchi wameishukuru Serikali kwani mradi huo ni ukombozi kwa wananchi wa Idofi na Kata kwa Ujumla kwani shule hiyo itawapunguzia mwendo wanafunzi, ambao kwa sasa wanatembea kilomita zisizopungua 20 kufika shule ya sekondari Mlowa, na kuwataka wananchi wa Kata hiyo kuwa wasimamizi na walinzi wa mradi na kuhakikisha wanazungumza lugha moja ili kutokwamisha mradi.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa