Na. Tanessa Lyimo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako Mhe.Salum Mlumbe amepongeza utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais kwa wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuleta fedha za miradi hali itayowezesha ukamilishaji wa miradi iliyoanzishwa na nguvu za wananchi na kutatua changamoto mbalimbali katika jamii.

Mhe. Mlumbe alitoa kauli hiyo januari 23,2026 katika ziara ya kamati ya Fedha na uongozi ya Halmashauri ya Mji Makambako ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha kuishia robo ya pili kwa mwaka wa fedha 2025/2026.

Miongoni mwa miradi iliyotembelewa ni pamoja na ujenzi wa Shule ya mpya ya Awali na Msingi katika eneo la shule ya Sekondari Mahongole kwa kupitia Serikali kuu chini ya mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa shule za Msingi (BOOST),Ujenzi wa madarasa 3 na matundu 7 katika Shule ya Msingi Lyamkena kupitia mradi wa Kuinua Uwezo wa Walimu katika Ufundishaji na Ujifunzaji (GPE-TSP),ukamilishaji wa Maabara katika shule ya Sekondari DeoSanga Kata ya Kivavi na Ujenzi wa Miundombinu ya Zahanati ya Mwembetogwa kupitia miradi ya Kupunguza umaskini (TASAF) pamoja na mradi wa vijana wa uatikaji wa Miche kupitia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kwa vikundi vya wanawake ,vijana na watu wenye ulemavu.



Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa