Na. Lina Sanga
Rai hiyo imetolewa leo na Mwl. Vicent Kayombo,Afisa elimu Mkoa wa Dodoma, akimuwakilisha Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI ,Dkt. Charles Msonde katika ziara ya kuongea na walimu wote nchini ikiwa ni pamoja na Mkoa wa Njombe.
Akiwasilisha maagizo ya Naibu Katibu Mkuu kwa walimu wa Halmashauri ya Mji Makambako,Mwl. Kayombo amewataka walimu kuwa watulivu kwani Serikali,kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI na Utumishi,wameshughulikia kero mbalimbali zilizokuwa zikiwakabili walimu wote nchini ikiwa ni suala la madaraja na miundo, ili kutatua kero hiyo mwezi julai,2024 walimu 54,000 wanapandishwa madaraja kwa mseleleko na walimu 52,000 wanapandishwa kawaida.
Amesema kuwa, kwa halmashauri ambazo mwezi julai,2024 mwalimu asipopandishwa daraja kwa sababu yoyote ile, Afisa utumishi atawajibika kwa kukiuka maagizo ya kuhakikisha walimu wote kuwa katika nafasi wanazotakiwa kuwa katika madaraja na miundo.
Pia, amewaagiza maafisa elimu kuhakikisha madeni ya malipo ya fedha za likizo na uhamisho zinalipwa kwa kuzingatia mtiririko,kwa kuanza kuwalipa walimu waliotangulia kudai fedha hizo badala ya kulipa madai mapya.
Aidha, amesisitiza suala la upendo baina ya walimu huku akiwataka maafisa elimu Kata kuwa viungo katika ya shule na mamlaka za juu,kuonyana kwa upendo na staha,kwa kutotoleana lugha zisizofaa na kusisitiza ubunifu katika ufundishaji ili kufanya mapinduzi katika sekta ya elimu kwa kuhakikisha matokeo mazuri yanapatikana.
Ametoa rai kwa wazazi na jamii kutambua umuhimu wa walimu kwani walimu wana jukumu la kusimamia malezi ya watoto wao,hivyo mwalimu anastahili kuheshimiwa, kuthaminiwa na kusaidiwa ili kurahisisha kazi yake ya malezi badala ya kupewa lawama zinazosababisha mwalimu kupoteza utulivu wa akili na kudhohofisha utendaji kazi wake.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa