Na. Lina Sanga
Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 ,zimeridhishwa na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji makambako,ikiwa ni pamoja na miradi inayotekelezwa na Serikali na watu binafsi pamoja na matumizi mazuri ya fursa zinazotolewa na Serikali.
Kauli hiyo imetolewa leo na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Ndg. Abdalla Shaibu Kaim katika ziara ya uzinduzi,ukaguzi na uwekaji wa jiwe la msingi katika miradi ya maendeleo,ikiwa ni pamoja na ujenzi wa madarasa mawili na ofisi moja shule ya msingi Mawande,Uhifadhi wa Msitu asili katika shule ya sekondari Mtimbwe,ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Ikelu,Shamba la Bi. Edda Sanga, mkulima wa mahindi aliyenufaika na pembejeo za ruzuku na jengo la hoteli la ghorofa la Bi. Benardetha Sanga na mradi wa kutengeneza chaki wa kikundi cha Youth Forum ambao ni wanufaika wa Mikopo ya asilimia 10.
Kaim, ametoa rai kwa vijana kujitokeza na kutumia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali,ikiwa ni pamoja na mikopo mbalimbali inayotolewa na Serikali ili waweze kujiajiri na kuwapongeza vijana wa kikundi cha Youth kwa uthubutu wa kuanzisha kiwanda cha utengenezaji chaki na kuiagiza Halmashauri kuwatafutia soko la bidhaa hiyo ili kukuza kipato na kufanya marejesho.
Pia,ametoa rai kwa wananchi wote kutumia vyandarua kujikinga dhidi ya malaria na kuwataka kina mama wajawazito na wenye watoto chini ya miaka mitano ,waliokabidhiwa vyandarua katika mbio za mwenge kuhakikisha wanatumia vyandarua hivyo kwa lengo lililokusudiwa na kuvitunza kwani vinatokana na kodi za wananchi.
Aidha,ametoa rai kwa wataalamu wa ujenzi kuwa makini katika utunzaji wa nyaraka za miradi na kutumia taaluma zao kuondoa gharama zisizo za msingi katika manunuzi ya vifaa,kwa kununua vifaa vinavyohitajika na venye ubora kwani fedha zinazotumika katika utekelezaji wa miradi ni kodi za Watanzania.
Mwenge wa uhuru 2023 umeongoza upandaji miti zaidi ya 500 na ugawaji wa vyandarua 100 kwa kina mama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano na kutembelea miradi sita yenye jumla ya 745 na kukimbizwa kilomita 50.6.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa