Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Makazi mheshimiwa Williamu lukuvi akiwa kama mgeni RASMI Katika ufunguzi wa maonesho ya NANENANE tarehe 01/8/2020 kwa nyanda za juu kusini mwa Tanzania ambapo maonesho hayo yanafanyika katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya ,katika hotuba yake fupi mh Lukuvi amesisitiza sana ulipaji wa kodi kwa ardhi ,Viwanja vyote lazima viwe na hati miliki ili kuondoa usumbufu kwa mmliki pindi unapotokea mgogoro wowote wa ardhi ,aidha amezitaka taasisi mbalimbali pia kuwa na hati miliki za mashamba na viwanja ,mfano magereza lazima wawe na hati miliki ya maeneo mbalimbli kwa lengo la kuepuka uvamizi kiholela .Mheshimiwa Lukuvi akachombeza kidogo kwa kauli mbiu ya maonesho ya nanenane ya mwaka huu "KWA MAENDELEO YA KILIMO ,UVUVI NA UFUGAJI CHAGUA VIONGOZO BORA 2020 " Ya kuwa kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu october 28 jamii inapaswa kuchagua viongozi makini kwa wakati sahihi ili waweze kuleta tija katika sekta mbalimbali hususani kilimo ,mifugo na uvuvi .
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa