Na. Lina Sanga
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka katika Mkutano wa Msemaji Mkuu wa Serikali na Idara ya Habari, Maelezo uliofanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Njombe kwa lengo la kuelezea utekelezaji wa shughuli mbalimbali uliofanywa na Serikali katika Mkoa wa Njombe na Halmashauri zake.
Mhe. Mtaka amesema maamuzi ya Rais kulipa fidia bil. 15 kwa ajili ya mradi wa liganga na mchuchuma katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ambao utekelezaji wake umechukua muda mrefu na ujenzi wa barabara ya zege ambayo itasaidia kumpunguzia majukumu mwekezaji ya kuboresha miundombinu na kulipa fidia wananchi.
Amesema kuwa Serikali ipo katika mchakato wa kumpata mwekezaji wa kuchimba makaa ya mawe,kujenga chemba ya kutenganisha chuma na madini yalipo kwenye chuma na, Ludewa ipo kwenye mazungumzo ya kupata mwekezaji wa pamoja kwa ajili ya ujenzi wa bandari ya kutoka Ludewa kwenda Mtwara na baada ya mradi huo kuanza kufanya kazi utabadili uchumi wa Mkoa wa Njombe na nchi kwa ujumla.
Aidha,amepongeza jitihada za Rais za kujenga miundombinu ya elimu,Afya na barabara ambapo katika ujenzi wa miundombinu ya elimu umepunguza kero kwa wananchi kuchangishwa fedha za ujenzi wa madarasa hasa nyakati hizi za maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza 2024.
Pia ,amepongeza uwekaji wa ruzuku kwenye mbolea ambayo kwa wananchi Mkoa wa Njombe ina tija,kwani wananchi wa Njombe wengi wanajishugulisha na kilimo na kwa sasa idadi ya wakulima imeongezeka.
Lakini pia, amempongeza Mhe. Samia kwa namna ambavyo chini ya uongozi wake fedha nyingi zinakuja kwa ajili ya utekelezaji wa miradi, na zinafanya kazi na mapungufu yanayoonekana ni ya watendaji na hatua zinachukuliwa.
Ametoa wito kwa watumishi wa Umma kuiweka Tanzania Mbele na kuzingatia uadilifu na uaminifu kwenye ofisi walizopewa kufanya kazi kwa kutofedhehesha taaluma zao kwa vitendo mbalimbali ikiwa ni pamoja na wizi wa dawa na vitendea kazi.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa