Na. Lina Sanga
Njombe
Kongamano la kuiombea nchi ya Tanzania na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan,kwa kazi kubwa nayoifanya ya kuliongoza taifa la Tanzania na kudumisha amani ya nchi.
Akizungumza na viongozi wa dini,viongozi wa kimila,viongozi wa Serikali na wananchi waliohudhuria kongamano hilo la maombi, lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Mji Njombe leo,Mhe. Waziri Kindamba ambaye alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe kabla ya kuhamishiwa Mkoani Songwe amesema kuwa sala na dua zilizofanyika kwa ajili ya Nchi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kutokana na kazi kubwa inayofanywa na Serikali kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kimkakati ambayo baadhi imekamilika na mingine ipo hatua ya ukamilishaji na mingine inaanza.
Mhe.Kindamba amesema kuwa,katika utawala wa Mhe. Samia Mkoa wa Njombe umepokea fedha za utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwa ni pamoja na bil. 136 kwa ajili ya ukamilishaji wa barabara ya Njombe na Makete,zaidi ya bil.179.2 kwa ajili ya ukamilishaji wa barabara ya Lusitu na Mawendi kwa kiwango cha zege na bil 95 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Itonyi na Lusitu.
Amesema kuwa jumla ya bil 3.3 kwa ajili ya mpango wa uboreshaji wa upatikanaji wa maji katika maeneo ya mijini na vijiji na jumla ya wananchi 24,880 watanufaika na mradi huo,baadhi ya wananchi wataonufaika na mradi huo wa maji ni katika vijiji vya Mlope,Ludewa mjini,Posta chini, Ngalanga, Sido, Matalawe, Ngelela na Isapulano.
Ameongeza kuwa jumla ya bil. 1,9 za tozo za miamala ya simu zilipokelewa ambapo mil. 150 zimetumika katika umaliziaji wa maboma ya madarasa kumi na mbili katika shule za Sekondari, bil 1.8 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vipya vya afya saba, zaidi ya bil. 4.7 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule za Msingi,Sekondari na shule shikizi.
Aidha amesema kuwa, manufaa makubwa yamepatikana kupitia fedha hizo zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya madarasa ni kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani,hivyo kutokana na juhudi za Mhe. Samia na Serikali yake ya awamu ya sita,Mkoa wa Njombe umeandaa maombi hayo maalumu ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Nchi kwa ujumla ili amani iliyopo iendelee kudumu daima.
Ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Njombe kuhakikisha wanapata chanjo ya Uviko 19 kwani hakutakuwa na usalama endapo jirani zao hawajapata chanjo,lakini pia amewataka wananchi wote wa Mkoa wa Njombe na Tanzania kwa ujumla,kujiandaa kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya watu na Makazi itakayofanyika kuanzia agosti 23,mwaka huu. Ili kupata takwimu sahihi kwa manufaa ya Umma.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa