Na. Lina Sanga
Tamko hilo limetolewa leo na Mhe. Deogratius Ndejembi,Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais -TAMISEMI alipokuwa akiwasalimia wananchi wa Mkoa wa Njombe,waliofika eneo la tanki la maji ,kwa ajili ya kumsikiliza Makamu wa RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akiwa safarini kuelekea Songea Mkoani Ruvuma.
Mhe. Ndejembi amesema kuwa,ili kuwapunguzia mwendo wanafunzi waliopo Kata ya Mjimwema,OR-TAMISEMI imepokea ombi la Mhe. Deo Sanga,Mbunge wa jimbo la Makambako la ombi la fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata ya Mjimwema ili kupunguza msongamano wa wanafunzi katika shule ya sekondari Deosanga na Makambako sekondari.
Amesema kuwa,baada ya kuhakikishiwa kupatikana kwa eneo la ujenzi wa shule hiyo,lililotolewa na kanisa la Romani katoliki Makambako,Wizara itatafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo ya Kata ya Mjimwema.
Naye,Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya makazi,Mhe. Geofrey Pinda ,ametoa rai kwa Halmashauri zote nchini,kuendelea kutenga ardhi ya akiba kwa ajili ya matumizi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo ya maziko na huduma mbalimbali pindi zinapohitajika.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa