Na. Lina Sanga
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka amewataka wafanyabiashara 112 wenye maghala na vizimba kurudi soko la mazao la Kiumba kuendelea na biashara ili kuwavutia wafanyabiashara wengine kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi.
Mhe. Mtaka ametoa wito huo leo katika kikao cha maridhiano kati ya Serikali na wafanyabiashara wa mazao,kilichofanyika katika uwanja wa ofisi ya Mkurugenzi katika Halmashauri ya Mji Makambako ,lengo kuu likiwa kujengeana uelewa ili matumizi ya soko hilo yaendelee kama ilivyokusudiwa.
Amesema kuwa, walengwa wakuu wa soko hilo ni wafanyabiashara wakubwa wa mazao na wanaohifadhi mazao kwenye nyumba za makazi ya watu na sio wafanyabiashara wadogo ambao wanauza kidogo kidogo kwenye masoko madogo na wakihitaji kufanya biashara katika soko la Kiumba wapewe nafasi.
Ameongeza kuwa, jukumu la wafanyabiashara kwa sasa ni kuhamia soko la Kiumba na kuendelea na biashara pasipo kumpangia mfanyabiashara mdogo eneo la kununua au kuuzia mazao, na Serikali ina jukumu la kuhakikisha malori yote ya mizigo yanashusha na kupakia mazao eneo la soko la mazao la kiumba na sio mahala pengine.
Ametoa rai kwa wafanyabiashara kuwa na kauli moja ili kufikia mafanikio,kwa kuacha uchochezi kwa kutumia wafanyabiashara wadogo ili kulinda maslahi yao binafsi ikiwa ni pamoja na wamiliki wa nyumba ambazo kwa sasa zinatumika kama stoo.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa