Na. Lina Sanga
Sekta zinazotoa huduma kwa jamii zimetakiwa kushirikiana katika kupanga matumizi ya ardhi kuepusha migogolo na wananchi.
Rai hiyo imetolewa leo na Mhe. Imani Fute, Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako katika mkutano wa baraza la Madiwani la kuishia kipindi cha robo ya tatu (januari -machi) 2023/2024,uliofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri.
Mhe. Fute amesema kuwa,ipo haja kwa mamlaka ,zote zinazohusika na utoaji wa huduma kwa wananchi,ikiwa ni pamoja na mamlaka za huduma ya maji, barabara na umeme ,kushirikiana pamoja na idara ya ardhi na mipango miji katika upimaji na upangaji wa ardhi,ili ijulikane barabara ilipo kabla ya mwananchi kufanya ujenzi.
Aidha, ametoa rai kwa Mkurugenzi na timu ya menejimenti kulichakata suala la ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata ya Mwembetogwa, baada ya Serikali kujenga shule mpya ya Azimio na eneo la awali kubaki na majengo chakavu.
Naye, Mkuu wa Wilaya ya Kipolisi Makambako, OCD Omary Diwani ametoa rai kwa jamii kushiriki katika kuzuia uhalifu na uvunjifu wa amani,badala ya kulitegemea jeshi la polisi pekee ,na kusisitiza jamii kuachana na imani potofu kwani kifo kipo na kila mmoja atakufa.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa