Na. Lina Sanga
Dar es salaam
Tamko hilo limetolewa na Waziri Mkuu,Mhe. Kassim Majaliwa katika ufunguzi wa kikao kazi cha 18 cha Maafisa habari,Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali, kilichofanyika leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.
Mhe. Majaliwa amesema kuwa ipo haja ya mamlaka mbalimbali kuwapa nafasi Maafisa Habari wa Serikali na Taasisi zote kuwa wasemaji wa taasisi kama ilivyo kwa klabu za mpira ili kuhabarisha umma kwa kutoa habari sahihi kwa wakati kuepusha upotoshaji.
"Nataka kuonyesha mfano ambao wenzetu wanafanikiwa mfano Msemaji wa Yanga kila siku tunamwona na Simba kila siku tunamwona ,Masao Bwire wa Ruvu shooting tunamuona kila siku hata wa Mtibwa kila siku tunamwona je, sisi? nimetoa mfano huu ili ndani ya siku tano za kikao hiki mfanye tathmini na Serikali ipo tayari kupokea ushauri wenu na kutekeleza matakwa yenu kama Maafisa habari",alisema Mhe. Majaliwa.
Aidha ametoa maagizo kwa Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Halmashauri na Taasisi zilizo chini ya Serikali kutambua umuhimu wa kuwa na Afisa habari katika taasisi na kukamilisha ikama ya Maafisa habari kama inavyohitajika pamoja na kutenga bajeti ya kutosha kwa ajili ya Vitengo vya Mawasiliano.
Pia,amewataka Viongozi wote kuwajengea uwezo Maafisa habari ili waweze kutumia teknolojia ya kisasa na kutengeneza utaratibu wa kuwashirikisha Maafisa habari katika utekelezaji wa shughuli zote za taasisi pamoja na miradi ya maendeleo kwa kuwawezesha vyombo vya usafiri wakati wa ziara za viongozi pamoja na kuwawezesha kushiriki vikao kazi.
Aidha, ameitaka Wizara ya Habari na Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na idara ya Habari Maelezo kuwasimamia na kuwakutanisha Maafisa habari kwenye vikao kupitia mitandao na ana kwa ana.
Kikao kazi cha 18 cha Maafisa Habari,Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kinafanyika kwa siku tano ambapo Maafisa hao watapata nafasi ya Kutembelea miradi ya Kimkakati inayotekelezwa na Serikali katika jiji la Dar es salaam machi 31,2023 siku ya Ijumaa.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa