• Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO
HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA OFISI YA RAIS TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Misingi Mikuu
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ardhi na maliasili
      • Raslimali watu na Utawala
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Usafi na mazingira
      • Elimu ya Msingi
      • Ujenzi na Uokoaji
      • Mipango na Ufuatiliaji
      • Elimu ya Sekondari
      • Kilimo, Ushirika na umwagiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maji
    • Vitengo
      • Sheria
      • ICT and Public relations
      • Ugavi na Manunuzi
      • Mkaguzi wa ndani
      • Ufugaji Nyuki
      • Uchaguzi
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma
    • Huduma ya Elimu
    • Huduma ya Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Uongozi
      • Huduma za Jamii
      • Kamati ya Maadili
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Mipango Miji na Mazingira
    • Ratiba
      • Ratiba ya kumwona Mwenyekiti wa Halmashauri
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyo kwenye Mpango
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Ripoti mbalimbali
    • Mikataba
    • Mpango Mkakati
    • Hatua
    • Fomu za maombi
    • Miongozo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Hotuba
    • Habari Mpya
    • Matukio
    • jarida la mji

SHULE SHIKIZI KUPEWA USAJILI RASMI

Tarehe iliyowekwa: December 19th, 2021

Naibu waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI,Mhe.David Silinde amewaagiza  Maafisa elimu idara ya msingi na sekondari,katika halmashauri ya Mji Makambako, kuhakikisha shule shikizi  zinapata usajili kuwa shule rasmi pindi ujenzi wa madarasa utapokamilika.

Mhe. Silinde ametoa agizo hilo leo,katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa madarasa inayotekelezwa kwa Fedha ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko 19, katika wilaya ya Njombe,ambapo katika halmashauri ya Mji  Makambako, amekagua mradi wa ujenzi wa madarasa matatu shule shikizi ya Mlumbe sekondari katika kata ya Lyamkena na ujenzi wa madarasa mawili shule ya msingi shikizi kihanga katika kata ya Mahongole.

Pia amewapongeza wananchi wa kata ya Lyamkena,kwa kutoa fedha kiasi cha shilingi mil. 24,kwa ajili ya fidia ya eneo ambalo limejengwa shule shikizi ya sekondari ya lyamkena inayotambulika kama Mlumbe sekondari,ambayo itasaidia kupunguza mlundikano wa wanafunzi katika shule  mama ya Lyamkena sekondari.

Aidha, Mhe. Silinde amemuagiza Mkurugenzi wa halmashauri ya Mji Makambako,Bw. Kenneth Haule kukamilisha madarasa na vyoo vilivyojengwa kwa nguvu ya wananchi katika shule ya msingi shikizi Kihanga,kwa kutumia mapato ya ndani ili shule hiyo ipate usajili kuwa shule ya msingi rasmi.

“Shule hizi shikizi kulingana na idadi ya madarasa yaliyopo,zina sifa ya kupata usajili kuwa shule rasmi ,hivyo maafisa elimu hakikisheni taratibu za usajili zinaanza kwa wakati na TAMISEMI itaongeza idadi ya madarasa mengine,pia halmashauri kupitia mapato yake imalizie majengo haya ya shule ya msingi shikizi kihanga yaliyojengwa kwa nguvu ya wananchi ili  kuunga mkono juhudi za wananchi”,alisema Mhe. Silinde.

Mwisho alitoa maelekezo kwa Uongozi wa halmashauri ya Mji Makambako kukamilisha majengo hayo kwa viwango na kuwa miradi yote ya ujenzi wa madarasa inayotekelezwa kwa fedha ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya Uviko 19, kukamilishwa ifikapo desemba 25,2021 ili kukabidhiwa kwa Mkuu wa wilaya na Mkuu wa Mkoa na hatimaye madarasa hayo kukabidhiwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Samia Suluhu Hassan.

Katika Halmashauri ya Mji Makambako, jumla ya shilingi mil.840 fedha ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko 19, ilipokelewa kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 26 pamoja na meza na viti kwa shule za sekondari na madarasa 12 pamoja na madawati kwa shule za msingi na bweni moja la wanafunzi wenye mahitaji maalumu shule ya msingi Idofi pamoja na vitanda.

Naye Katibu Tawala  Mkoa wa Njombe,Judica Omary ametoa shukurani kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kwa fedha ya ujenzi wa madarasa kwani kupitia fedha hiyo Upungufu wa madarasa kwa sasa umepungua,na wanafunzi wataingia darasani mwezi januari kwenye madarasa yaliyokamilika na yenye meza na viti pamoja na madawati kwa upande wa shule za msingi.

 

Matangazo

  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 13 April 19, 2025
  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 12. April 20, 2025
  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 11. April 21, 2025
  • Ujio wa Mwenge wa Uhuru 2025, bado siku 10. April 22, 2025
  • Fungua

Habari Mpya

  • Wataalamu na viongozi watakiwa kusimamia upatikanaji na utoaji wa huduma za chanjo.

    April 25, 2025
  • Makambako yang'ara katika tuzo za Afya ya Usafi wa Mazingira ngazi ya Halmashauri za Miji.

    April 09, 2025
  • Jumla ya Miti 15,000 kupandwa Halmashauri ya Mji Makambako kuelekea siku ya Miti duniani mwaka 2025.

    March 15, 2025
  • Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani 2025 Mkoa wa Njombe, Mila kandamizi zaelezwa kuwa kikwazo cha ustawi na uwezeshaji

    March 09, 2025
  • Fungua

Video

Shule mpya ya Mbugani Kitandililo sekondari kupitia mradi wa SEQUIP
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Fursa za Usafirishaji
  • Orodha ya Madiwani
  • Uzalishaji wa Umeme wa Upepo
  • Organisation Structure
  • Fursa za Biashara
  • By Laws
  • Permanent Committee

Tovuti Mashuhuri

  • Tovuti ya Ikulu ya Rais
  • Tovuti ya Ofisi ya Utumishi
  • Tovuti ya TAMISEMI
  • Tovuti ya Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS)
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Open Data Tanzania

Wasomaji mbalimbali duniani

world map hits counter

Idadi ya Wasomaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Makambako Town Council

    Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako

    Simu ya mezani: 026-2730044

    Simu ya Kiganjani: 0785635383

    Barua pepe: td@makambakotc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa