Na. Lina Sanga
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako, Kenneth Haule mara baada ya kupokea malalamiko ya wafanyabiashara wa mazao katika soko la Kiumba,kutokana na baadhi ya wafanyabiashara kukaidi agizo la kuhamia katika soko hilo.
Haule ,amesema kuwa Ujenzi wa soko la mazao la Kiumba ni moja kati ya mipango mingi ya upangaji wa Mji kutokana na Mji kukua kwa kasi,hivyo wananchi wote ndani ya Makambako wanawajibu wa kukubali na kushirikiana na Serikali katika kuboresha Mji kwa maslahi ya Wakazi wa Makambako.
Amesema kuwa, Makambako inapokea wawekezaji mbalimbali wenye nia ya kufanya uwekezaji Mkubwa hususani Viwanda,hivyo zoezi la kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli mbalimbali ni muhimu Kutokana na Mji kukua kwa kasi hivyo wananchi wawe tayari kupokea mabadiliko kwa mtazamo chanya badala ya kuibua vikwazo visivyo na tija.
Ametoa rai kwa wafanyabiashara wa mazao ambao wamekaidi kuhamia katika soko la Kiumba na kuendelea kufanya biashara maeneo yasiyo rasmi,kuhakikisha wanahamia na kufanya biashara zao katika Soko husika ndani ya masaa 72,kwani katika Mji wa Makambako soko la mazao ni moja tu ambalo ni soko la mazao la kiumba.
Aidha,amewataka wafanyabiashara wa mazao ambao tayari wamehamia katika soko hilo kuwa na subira,hali ya soko itatengamaa na biashara zitafanyika na watapata faida endapo wafanyabiashara wote watafanyia biashara eneo moja,Serikali inaendelea kuboresha miundombinu kuhakikisha biashara zinafanyika.
Naye, Mkuu wa polisi wa Wilaya ya Kipolisi Makambako,OCD Omary Diwani amewataka wafanyabiashara wote waliosalia katika maeneo yasiyo rasmi,kufunga biashara zao au kuhamia katika soko husika,badala ya kuwa kikwazo cha kukwamisha jitihada zinazofanya na Serikali, na yeyote anayekaidi kuhama atahamishwa kwa lazima kwani atakuwa tofauti na azma ya Serikali.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa