Pichani ni viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Madiwani na Watendaji wa Serikali katika Halmashauri ya Mji wa Makambako na Wilaya kwa ujumla katika mkutano wa taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Mapinduzi 2020/2021,ambayo imewasilishwa kwenye Mkutano Mkuu wa jimbo la Makambako Katika kikao hicho kwa pamoja watendaji wote wametakiwa kusimamai fedha zinazotolewa na serikali kwaajili ya kutatua kero na changamoto mbalimbali za maendeleo katika jimbo la Makambako hasa katika sekta ya elimu, afya na miundombinu ya barabara.
Akizungumza na hadhara Mbunge wa jimbo la jimbo la Makambako Deo Sanga wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Green city Makambako amesema serikali katika mwaka wa fedha 2020/2021imeendelea kutoa fedha nyingi katika miradi mbalimbli ikiweo miradi ya Maji kata ya Utengule kata ya Kitandililo na Mahongole pamoja na fedha kwaajili ya ujenzi wa sekondari ya kitisi.
Ameongeza kuwa ni wajibu wa viongozi wote wa Chama ,Madiwani na watendaji wa Halmashauri kusimamia ipasavyo fedha za serikali ambazo zimepangwa kutumika katika miradi ambayo imekusudiwa kinyume na hapo basi nafasi hizo haziwatoshi.
Akisoma taarifa mbele ya mkutano huo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Makambako, Paulo Malala amesema Halmashauri inaendelea na ujenzi wa miundombinu mbalimbali kwa sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shuleya sekondari Makambako, Deo Sanga,Maguvani na Mtimbwe sekondari.
Aidha kwa changamoto mbalimbali ambazo zimeibuliwa na wajumbe katika mkutano huo hasa katika miundombinu ya barabara ,umeme kwa pamoja zimeahidiwa kufanyiwa kazi kwa wakati hususani kwa upande wa barabara ya Maguvani Kifumbe ambapo mhandisi, Anyetili kasongo amesema kwa mwaka wa fedha 2021/2022 barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha kokoto.Wakati huo kwa kipindi cha miaka mitano mbunge wa jimbo la Makambako Deo Sanga amechangia fedha zake zaidi ya shilingi Milion Mia Tano sabini na Tano kwenye miradi mbalimbali ya maendeleo ya katika jimbo la Makambako ,ambapo amesisitiza suala la kujitoa kwa hali na mali katika maendeleo ya wananchi kwani ukiwa na pesa nyingi haaminishi utazikwa nazo fedha utaziacha ni vema kuweka alama katika jamii zetu tukiwa hai
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa