Na. Lina Sanga
Tamko hilo limetolewa leo na Bw. Agathon Kipandula,Meneja utawala na fedha wa Benki Kuu ya Tanzania kanda ya Mbeya,katika semina kuhusu utaratibu wa minada ya dhamana za Serikali pamoja na faida zake iliyofanyika katika Ukumbi wa greencity na kuhudhuriwa na baadhi ya wafanyabiashara na timu ya menejimenti ya Halmashauri ya Mji Makambako.
Kipandula,ametoa tamko hilo baada ya Mwenyekiti wa jumuiya wa wafanyabiashara Mkoa wa Njombe, Sifael Msigala kuhoji usimamizi na udhibiti wa taasisi za kukopesha fedha maarufu kama Kausha damu,kutokana na adha mbalimbali wanazopitia wananchi baada ya kukopa kwenye taasisi hizo.
Kipandula amesema kuwa, jukumu moja wapo la benki kuu ya Tanzania ni kusimamia benki zote ikiwa ni pamoja na kausha damu,ila kutokana na sababu mbalimbali za kiutendaji kausha damu bado hazijafikiwa na benki kuu hivyo ili kurahisisha usimamizi na udhibiti wa ukiukwaji wa sheria za fedha jukumu hilo linakabidhiwa kwa Wakurugenzi wa Halmashauri husika.
Amewataka wananchi kutoa taarifa za kudhulumiwa na kausha damu kwa kuwa na ushahidi ,pamoja na fedha ambazo zilikuwa kwenye kadi za simu zilizopotea au kuharibika na kutotumika tena kupitia dawati la usuluhishi wa miamala la benki kuu ya Tanzania,ili warejeshewe fedha zao kwani miamala yote ya kifedha inasimamiwa na benki kuu na siyo TCRA kwani jukumu lake ni moja tu,la mawasiliano.
Amebainisha kuwa, hadi kufikia leo aprili 9,2024 jumla ya bil. 40 zimepatikana kutoka kwenye kadi za simu zilizotupwa au kupotea na wamiliki kutofanya ufuatiliaji wa kurejeshewa fedha hizo.
Awali akifungua semina hiyo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Makambako,Kenneth Haule ameipongeza benki kuu ya Tanzania kwa kuandaa semina hiyo yenye manufaa kwa wananchi wote,ikiwa ni pamoja na watumishi wa Umma.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa