Na. Lina Sanga
Kauli hiyo imetolewa na Bi. Christina Mangula (60) mkazi wa Kitongoji cha Itofoga,Kijiji cha Ibatu katika Kata ya Kitandililo mnufaika wa TASAF tangu mwaka 2015 na kubainisha kuwa,kabla ya kufikiwa na TASAF hali ya maisha ilikuwa ngumu sana kwani hata uhakika wa chakula ulikua mdogo,lakini baada ya TASAF kumpa mradi wa mbuzi maisha yalibadilika mpaka sasa ana uhakika wa chakula,mavazi na matibabu.
Amesema kuwa baada ya kukabidhiwa mbuzi tatu dume moja na mbuzi jike wawili ambao walizaa mbuzi wengine watatu,na aliuza mbuzi wawili na kununua bati kwani nyumba aliyokuwa akiishi awali ilikuwa imeezekwa kwa nyasi na nyakati za mvua ilikuwa inavuja.
“Nilifanikiwa kuwatunza mbuzi niliopewa na wakazaliana uzao wa kwanza nikaamua kuuza wawili kila mmoja shilingi 50,000 na kununua bati kwa ajili ya kuezeka nyumba niliyoachiwa na mume wangu kabla hajapatwa na umauti,maana ilikuwa inavuja sana”,alisema Bi. Christina.
Ameongeza kuwa,licha ya mradi huo wa ufugaji wa mbuzi pia anafanya shughuli za kilimo cha mahindi,maharage na bustani ya mbogamboga kwa ajili ya matumizi ya nyumbani,na kwa sasa ana chakula cha kutosha hivyo uhakika wa kula upo.
Ametoa rai kwa wanufaika wote wa TASAF nchini kujifunza kwa wanufaika wengine waliofanikiwa ili kuunga mkono juhudi za Serikali,za kutokomeza umasikini na kuboresha hali ya maisha kwa kaya masikini.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa