Na. Lina Sanga
Bi. Zabela Simangwa mkulima na mfugaji katika Kijiji cha Mawande,Kata ya Utengule katika Halmashauri ya Mji Makambako ameishukuru Serikali kwa kumuwezesha kupitia fedha za Mfuko wa Maendeleo ya jamii TASAF zilizomuwezesha kufanya shughuli za kilimo cha mahindi,alizeti na ufugaji wa kuku na nguruwe.
Bi. Zabela amesema kuwa,mwaka 2015 kupitia mpango wa TASAF wa kunusuru kaya masikini alifanikiwa kupata shilingi 20,000 ambazo hutolewa kila baada ya miezi 2,na zinamuwezesha kuweka akiba katika kikundi cha maendeleo cha TASAF na kufanikiwa kununua bati na mbao na kuezeka nyumba yake iliyokuwa ya nyasi aliyoijenga mwaka 1998.
Amesema kuwa,mwaka 2017 kupitia TASAF alipewa mradi wa kufuga nguruwe na alikabidhiwa nguruwe jike na dume,ambazo zilimuwezesha kuongeza kipato kwa kuuza vitoto na kukodisha nguruwe dume wa kupandikiza na kupewa kitoto kimoja kwa kila nguruwe aliyepandwa na nguruwe wake.
“Nilikodisha nguruwe dume kwa watu sita kwa ajili ya upandikizaji na baada ya nguruwe hao kuzaa nilipata jumla ya vitoto sita ambavyo niliuza vitano kwa shilingi 50,000 na nguruwe mkubwa nilimuuza kwa shilingi laki 280,000 na kubakiza dume moja kwa ajili ya mbegu,kwa sasa nina nguruwe majike mawili na dume moja”,alisema Bi. Zabela.
Kwa upande wa kilimo,Bi. Zabela amesema kuwa amefanikiwa kulima shamba ekari 2.5 ambapo ekari 1.5 analima mahindi na ekari 1 analima zao la alizeti,hivyo ana uhakika wa chakula kwa msimu wote tofauti na zamani chakula kilipatikana kwa shida,na kwa sasa anatarajia jitihada kukarabati nyumba,kujenga choo cha kisasa na tayari nimeanza maandalizi.
Katika kijiji cha Mawande kuna jumla ya vikundi vinne vya Maendeleo vya kuweka na kukopa vya wananufaika wa Mfuko wa Maendeleo wa TASAF, ambavyo kwa nafasi kubwa vimewawezesha wanufaika wengi kuinuka kiuchumi na kubadilisha maisha yao.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa