Mashine ya kukamua Mafuta ya Alizeti inayomiikiwa na kikundi cha Faraja kinacho miikiwa na wanawake katika kijiji cha Mawande Halmashauri ya Mji wa Makambako ambapo wamepata fursa ya kutembelewa na wakaguzi kutoka Maendeleo ya jamii TAMISEMI zoezi lililoongozwa na Hilda mgomapayo ,huku wakitaka kujua ni kwa naman gani mkopo uliotolewa na serikai kwa kikundi hicho kupitia Halamshauri ya Mji wa Makambako umesaidiaje Wanawake kama walengwa wa mkopo huo .Wakizungumza na afisa Maendeleo ya jamii TAMISEMI Katika Risala yao fupi wamesema kuwa wamenufaika na mkopo huo uliotolewa mwezi wa tisa ambapo kiasi cha shilingi Million kumi zilitolewa na tayari wamesharejesha laki saba mbali na hayo wamesaidia jamii ya kijiji hicho kutoenda umbali mrefu kwaajili ya kupata huduma ya kuchuja mafuta ,na pia wamesaidia jami ya kijijini hapo kupata chakula cha mifugo kwa masalia mara baada ya kuchuja mafuta hayo hususani Mashudu .Wameishukuru Halmashauri ya Mji wa Makambako kwa msaada wao wa kuwatembelea na kuwapa elimu juu ya ujasiriamali na kuwapa elimu nzuri namna ya kurejesha mkopo huo kwa wakati mwafaka.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa