Katika picha ni zoezi la ukaguzi wa vikundi mbalimbali uliofanywa na idara ya maendeleo ya jamii ya Halmashauri ya Mji wa Makambako kwa kushirikiana na maendeleo ya jamii TAMISEMI ambapo kikundi cha Muungano kilichopo maeneo ya kitisi Makambako ni mmoja ya kikundi nufaika na Mkopo wa serikali kupitia Halmashauri kikiwa chini ya wanawake kimenufaika na Mkopo kutoka serikalini kupitia Halmashauri ambapo takribani fedha za kitanzania takribani (Millioni kumi ) zilitolewa mwezi wa kumi kwa kikundi hicho .Mnamo tarehe 30 Decemba kikundi hicho kilitembelewa na wakaguzi kutoka TAMISEMI huku mkuu wa msafara huo akiwa ni Hilda Mgomapayo wakati lengo kubwa likiwa ni kujua ni kwa namna gani fedha hizo zinatumika na kuwapa manufaa walengwa na ni kwa jinsi gani zinarejeshwa kwa wakati kama ilivyopangwa .wakiongea mbele ya Afisa maendeleo ya jamii TAMISEMI wamekiri kuwa mkopo huo umewanufaisha kwa kasi kubwa hasa katika mradi wao wa kusindika Mvinyo wa matunda Matatu (nyanya ,limau na Chungwa ) na kuwa tayari soko la mvinyo huo limeenda mbali zaidi takribani Mikoa mingi Nchini na soko lake ni la uhakika. kwa upande mwingine hawakusita kuishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kazi nzuri hasa kuhimiza vijana ,Wanawake,na walemavu kujikita katika ujasiriamali na uzalishaji kupitia mikopo mbalimbali inayotolewa na serikali ,
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa