Mwenge wa uhuru ulipokelewa katika halmashauri ya mji wa Makambako mnamo tarehe 15 Septemba 2019.Mwenge huo ulifanikiwa kumulika miradi mitano(5) ya maendeleo na kuifungua
Miradi hiyo ni kama ifuatavyo:
1.UJENZI WA MAJENGO 7 YA HOSPITALI YA HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO.
Hospitali hiyo ina hadhi ya hospitali ya wilaya ambayo itakuwa ikiwahudumia wananchi zaidi ya 100,000 wa ndani na nje ya halmashauri ya mji wa Makambako.
Ujenzi huo ni miongoni mwa miradi 67 ya hospitali za wilaya unaoendelea nchi nzima.
2.UJENZI WA VYUMBA VIWILI VYA MADARASA NA CHUMBA KIMOJA CHA OFISI KATIKA SHULE YA MSINGI IDOFI.
Mradi huu umegharimu Jumla ya sh.37,980,000/= kwa ushirikiano wa wananchi,mbunge na serikali
kwa mchanganuo ufuatao
a)Ruzuku toka Serikali kuu (EP4R) Awamu ya kwanza mwaka 2017 Tshs. 1,000,000.00
b)Ruzuku toka Serikali kuu (EP4R) Awamu ya pili mwaka 2019 Tshs. 25,000,000.00
c)Mhe. Mbunge Deo sanga Tshs. 300,000.00
d)Mhe. Diwani Festo Mwalongo Tshs. 120,000.00
e)Nguvu za Wananchi Tshs. 10,780,000.00
f)Mfuko wa Jimbo Tshs. 780,000.00
3.UJENZI WA VYUMBA 2 VYA MADARASA, OFISI MOJA YA WALIMU NA MATUNDU 8 YA VYOO SHULE YA SEKONDARI LYAMKENA
Mradi wa Ujenzi vyumba 2 vya Madarasa,Ofisi 1 ya walimu na matundu 8 ya vyoo Shule ya Sekondari Lyamkena unatekelezwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).
Mfuko wa TASAF Kitaifa unalenga kupunguza umasikini katika jamii. Kwa sasa Mradi wa Kupunguza umasikini katika Nchi yetu unatekelezwa chini ya Programu ya OPEC III.
Aidha, mradi huu pia umejikita katika kuboresha huduma za jamii katika Sekta za Elimu na Afya mahali palipo na upungufu
4.MRADI WA KIWANDA CHA KUKUNJA BATI (HEROCEAN ENTERPRISES (T) LTD AINA YA DRAGON
Madhumuni ya kuanzishwa kiwanda hiki cha kukunja bati ni kutekeleza azma ya uchumi wa kati wa viwanda kwa ajili ya kukuza uchumi na kuongeza kipato kwa wananchi na kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu ifikapo 2030
5.MRADI WA UJENZI WA JENGO LA UPASUAJI MDOGO KATIKA HOSPITALI YA MT. JOSEPH IKELU
Malengo ya mradi huu wa ujenzi wa jengo hili huduma ya upasuaji mdogo ulibuniwa kutokana na uhaba mkubwa vyumba vya kutolea huduma hii pamoja na huduma ya dharura kabla mgonjwa hajapelekwa wodini kupata huduma zaidi.
Miradi yote ilipitishwa na kufunguliwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Ally na kusifia kazi nzuri inayofanywa na halmashauri ya mji wa makambako chini ya mwenyekiti Mh.Chesko Hanana Mfikwa na Mkurugenzi Ndugu Paulo Malala katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa