Pichani ni Miti ya Makambako yenye asili ya jina Makambako maana yake ni: Ng"ombe Dume (Fahari) ambao waliletwa kwaajili ya kuchinjwa kwenye Matambiko yao wakati chifu Mkwawa akiwa ameitisha kikao chake katika harakati za kulinda mipaka ya eneo la utawala wake lisivamiwe wakatio wa vita vya makabila kati ya chifu Mkwawa na Chifu nduna wa Songea ,sasa kutokana na kuzoeleaka kwa zoezi la uletaji fahari hao ikapelekea neno Makambako kutamkwa kila wakati na mahali hapo mpaka leo huitwa Miti ya Makambako ambapo jamii inawajibu wa kutunza historia hii ili iwe somo hata kwa vizazi vya baadae
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa