Na. Lina Sanga
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt Philip Isdor Mpango leo amezindua mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2022 Mkoani Njombe,na kuwataka wananchi wote nchini kujiandaa kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya watu na makazi,kwa kutoa taarifa sahihi ili kufanikisha azma ya taifa kuwa na taarifa sahihi na za muhimu kwa maendeleo endelevu na kuwa taarifa zote zitakuwa za siri na kutumika kwa madhumuni ya takwimu pekee.
Pia amewataka viongozi wote na waratibu wote wa sensa kuwaandaa wananchi wote nchini,ili waweze kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa kwa kutoa elimu juu ya umuhimu wa sensa,miongozo na taratibu zitakazo wezesha utekelezaji wa zoezi hilo kikamilifu na kuhakikisha wanafanikiwa kumuhesabu kila mwananchi mara moja tu.
Aidha Dkt. Mpango ametoa msisitizo kwa wananchi wote kuendelea kuchukua tahadhari juu ya maambukizi ya Upungufu wa Kinga Mwilini (UKIMWI), kupinga matumizi ya madawa ya kulevya,kupinga rushwa na kuwakuwakumbusha Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU ),kutekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan la kukamilisha uchunguzi wa miradi 54 iliyotiliwa shaka kwenye mbio za mwenge wa uhuru wa mwaka 2021 na endapo kuna ushahidi wa kutosha watuhumiwa wote wafikishwe mahakamani
Ametoa wito kwa wakimbiza Mwenge Kitaifa kutozindua kila mradi ili kukamilisha ratiba,bali wazingatie miradi yote watayozindua inalingana na thamani ya fedha zilizotumika na kutoa taarifa kwa vyombo vinavyohusika kwa miradi yote watayotilia mashaka ili uchunguzi ufanyike na hatua za kisheria zichukuliwe.
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa kwa mwaka huu ni Ndg.Sahili Nyanzabara Geraruma(Njombe) ambaye ndiye kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu,Rodrick Romward Ndyamukama (Mwanza),Zadida Abdalla Rashid(Kusini Pemba),Gloria Festo Peter (Singida), Ali Juma Ali(Mjini Magharibi),Emmanuel Ndege Chacha(Kagera).
Makambako Town Council
Anuani ya Posta: P.O.BOX 405 Makambako
Simu ya mezani: 026-2730044
Simu ya Kiganjani: 0785635383
Barua pepe: td@makambakotc.go.tz
Haki miliki ©2017 Halmashauri ya Mji Makambako. Haki zote zimehifadhiwa